NAIBU WAZIRI AMOSI MAKALA; “ Sanaa na utamaduni kuleta ajira”
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
NAIBU Waziri wa
Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala amesma Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea
kuenziwa ili kuwaleta ajira vijana pindi watakapokuwa tayari kuienzi kwa
vitendo na kuisomea.
Makala alisema hayo mjini hapa alipokuwa mgeni rasmi kwenye
ufunguzi wa tamasha la 32, la Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo lenye kauli mbiu ‘Sanaa na Utamaduni katika kukuza utalii’
linaloshirikisha vikundi zaidi ya 70, kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Akihutubia, umati wa wananchi,wanafunzi wa chuo hicho cha
sanaa na vikundi mbalimbali vinavyoshiriki, Waaziri Makala alisema akiwa waziri
mwenye dhamana atahakikisha utamaduni na sanaa nchini inakua huku ikiwanufaisha
watu wote kwa vizazi vya sasa na vya
baadae.
“Katika kuenzi Sanaa na
Utamaduni, Wizara ina mipangilio mingi ikiwemo nay a kuakikisha tunakuza
utamaduni wa Taifa letu na hata ajira kwa vijana ambao watajiunga na sanaa
hivyo tutaendelea kushirikiana na chuo cha TasuBa na wadau wengine katika kufikia malengo”
alisema Makala.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Michael
Kadinde alisema watahakikisha tamasha hilo kongwe nchini wanafikia
vikundi na wasanii mbalimbali ilikupata kushiriki na kuonesha
kazi zao.
“Lengo kufikia wasanii wote na hilo tunafanya kila mwaka na
zaidi milango ipo wazi kwa mashirika binafsi ya ndani na nje kuja kuwekeza na
kukuza sanaa zetu” alisema Kadinde
Na kuongeza kuwa kwa sasa TaSUBa ina enzi na kulithisha
sanaa na utamaduni kwa vitendo ikiwemo kutoa mafunzo kwa watoto wadogo na wale wa
elimu ya msingi.
..
Kwa upande wa Vikundi vinavyoshiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja
na ;
Alisema, vikundi 40 kati ya 60, ni kutoka Tanzania na
vingine ni kutoka nje ya nchi vikiwemo vilivyowahi kushiriki tamasha hilo na vipya
ambavyo itakuwa ni mara ya kwanza kuja.
Alivitaja vikundi vya Tanzania kuwa ni Ngome International
Magic Show – JWTZ, Splendid Theatre,
Kigamboni Community Centre, Malezi Youth Theatre na Jivunie Tanzania Sanaa.
Vingine ni Mapoloni Culture Centre, Albino Revolutionary,
Cocodo African Music, Imani Theatre, Safi Theatre, Imara Boma, Bagamoyo House
of Talents, Bwagamoyo Africulture, Godykaozya & Tongwa Band na Mtoto
Mchoraji.
Vimo pia Shada Acrobatics, Bagamoyo Players, Bayoice,
Jikhoman & Afrika Sana Band, Vitalis Maembe & The Spirit Band na
Bagamoyo Dance Company.
Aidha, kuna vikundi vya Makini Organization (Arusha),
Tumaini Group (Manyara), Kimanzichana Vijana Group (Mkuranga), Utandawazi
Theatre Group (Matwi Gha Chalo), kutoka visiwa vya Ukerewe, Hiari ya Moyo
(Dodoma), Moshi Police Academy (Moshi), CBM Acrobatic Group, Man Kifimbo Band
na Midundo ya Sanaa. Pia kuna vikundi kutoka Ethiopia , Kenya , Norway , Uganda
, Rwanda na Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment