BAADHI ya walimu wa shule za msingi wamefurahishwa na serikali kuanzisha mtihani wataifa wa darasa la pili kuwa itasaidia kutiliwa mkazo kwa elimu ya awali na kuongeza ufaulu katika mitihani ya darasa la nne.
Aidha,amebainisha kuwa mtihani huo ikiwa utatiiliwa mazona wizara ya elimu ipasavyo tatizo wanafunzi kutojua kusoma au kuandika itakuwa ndoto.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mkoani Jane Mganwa alisema wamefurahishwa na mpango huo ambao wanaamini utasaidia walimu wa madarasa la kwanza na pili kuongeza juhudi pamoja na wanafunzi wenyewe ili kuepuka kufeli.
Alisema kwani kuna baadhi ya wazazi hawaoni umuhimu wa elimu hiyo na kufanya wanafunzi kuwa mzigo kwa walimu wa darasa la kwanza na pili ambao kwa sasa hawafundishi kusoma na kuandika.
“kwa sasa madarasa hayo mawili wanafundisha masomo saba na siyo uumbaji wa elimu au kusoma hivyo sasa kwa kuwepo mtihani huu watoto watapelekwa shule ya awali”alisema
Naye mwalimu wa Taaluma toka shule ya msingi Vetenary,Amina swai alisema mpango huo utakuwa changamoto kwa wazazi na walimu kutilia mkazo katika kutoa mafunzo na ufuatiliaji ili kuepuka wananfunzi na watoto wao kurudia rudia darasa moja.
Lakini ,Rais wa Chama cha Walimu (CWT)Gratian Mukoba alisema mitihani hiyo ingebakizwa kwa walimu kuchuja kwani kuwepo kutaongeza mzigo kwa wazazi.
Alisema wazazi watakuwa na mizigo ya kulipia mtihani wa darasa la pili,nne,saba,Kidato cha pili na kidato cha nne hivyo walimu wangepewa tamko tu kuwa wasiojua kusoma na kuandika wasivuke darasa la pili.
Juzi ,Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo alisema serikali inatarajia kuanziha mtihani mpya wa Taifa kwa wanafunzi wa darasa la pili nchi nzima ili kuchuja watakaoshindwa kusoma,kuandika na kuhesabu.
Alisema mtihani huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa katika sekta ya elimu kwa lengo la kuondoa uwezekano wa kuwa na wanafunzi katika madarasa ya juu wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu.
Alisema ili kufikia malengo hayo watakaoshindwa mtihani huo watarudia mpaka wajue kusoma na kuandika
Mwisho
0 comments:
Post a Comment