Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea kufurahishwa kwake na huduma hiyo |
Mtaaalamu wa Bidhaa wa simu kampuni ya simu ya Zantel Cecil Mhina akifafanua
namna ya upatikanaji wa taarifa za kilimo kupitia mtandao huo, pembeni yake ni
Afisa Rasirimali Watu Mkuu wa Zantel Francis Kiaga na Mkurugenzi wa Kilimo
katika Wizara ya Kilimo na Ushirika Mshindo Msola na Mkurugenzi Mkuu
wa kampuni ya Sibesonke inayoratibu taarifa hizo, Uwe Schwarz,. ( Picha
na Mpiga Picha Wetu)
Na Mdau wa Elimuboratanzania
Kampuni
ya simu za mikononi ya Zantel, kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika pamoja na kampuni ya Sibesonke leo wamezindua huduma mpya ya kutoa
taarifa kuhusu kilimo kupitia simu za mikononi.
Huduma
hiyo mpya inayofahamika kama,Z-KILIMO,itawawezesha wakulima nchini Tanzania
kupata taarifa za papo kwa pao na uhakika kuhusu njia za kuendesha kilimo cha
kisasa kwenye simu zao za mikononi.
Kupitia
huduma hii ya Z-KILIMO, wakulima nchini, hata wale walio vijijini wataweza kupata
taarifa muhimu za namna ya kuendesha kilimo cha kisasa na hivyo kuongeza
uzalishaji na kukuza sekta nzima ya kilimo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel,
Francis Kiaga, amesema kwa kupitia huduma hii wakulima nchini watapata fursa ya
kipekee kupata taarifa kuhusu kilimo moja kwa moja kupitia simu zao.
“Kilimo
ni uti wa mgongo wa uchumi wetu, na kinachangia sana kwenye kukuza na kuchangia
uchumi wa nchi yetu, na huduma hii imekuja wakati muafaka katika kuendeleza
juhudi hizo, lakini pia kuwapa wakulima umuhimu wa huduma ya simu katika namna
wanayoihitaji zaidi’ alisema Kiaga.
Akielezea
zaidi huduma hiyo Kiaga alisema itawasaidia zaidi wakulima katika kuokoa muda
ambao zamani waliupoteza katika kupata taarifa kuhusu kilimo, na pia
kuwaongezea uzalishaji wa mazao yao.
Huduma ya
Z-KILIMO pia itawapa wakulima taarifa kuhusu maandilizi ya ardhi, aina za
mbolea, aina za mazao, aina za mifugo, aina ya magonjwa yanayoshambulia mazao,
upaliliaji, taarifa za usafiri, hali ya hewa pamoja na sehemu ya majadiliano
baina ya wakulima.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea
kufurahishwa kwake na huduma akisema itasaidia kufungua fursa zaidi kwa
wakulima nchini.
‘Kupitia
huduma hii, wakulima sasa wataweza kuboresha mbinu zao za kilimo katika hatua
zote za kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji’ alisema Dkt Msola.
Nao
kampuni ya Sibesonke, ambao wameingia ushirikiano wa kiteknolojia na wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na wizara ya maenedeleo ya Mifugo na Uvuvi,
ukiwa na lengo la uwafikia watanzania wakulima kuwapa taarifa muhimu za kilimo
kwenye simu zao.
“Sibesonke
ina furaha kwa kuwezesha watanzania kufaidika na teknolojia hii kupitia mtandao
wa Zantel’ alisema Daktari Uwe Schwarz, Mkurugenzi Mkuu wa Sibesonke. “Kampuni
ya Zantel imeonyesha dhamira ya dhati katika kuhakikisha teknoljia hii
inawafaidisha watanzania wote kwa mtandao wake ulioenea nchi nzima’ alisiistiza
Daktari Schwarz.
Wakulima
wanaweza kujiunga na huduma hii kwa kubonyeza *149*50#, ambapo wataweza kupata maelekezo ya kutumia huduma hii.
0 comments:
Post a Comment