Furaha ilioje |
Shafi Majaar akitoa hotuba yake |
Wakaimba nyimbo za shukrani |
Manyanya akizindua madawati kwa kuandika |
Zena Majaar Tenga ambae ni Mkurugenzi wa HMT akisoma risala yake |
Picha ya pamoja |
Wanafunzi wakifurahia msaada huo |
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa shukrani zake |
Sharif Maajar akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stela Manyanya uthibitisho wa utoaji wa madawati hayo (asante Hamza Temba wa ofisi ya RC Rukwa).
Habari kwa hisani ya HMT
Taasisi ya Hassan Maajar Trust imetoa
msaada wa madawati 321 katika shule nane (8) katika Halmashauri nne (4) za mkoa
wa Rukwa yatakayokalisha wanafunzi 963.
Madawati hayo yalikabidhiwa katika
hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi ya Kansense, iliyoko Wilaya ya
Sumbawanga. Bi Zena M Tenga pamoja Bwana Shariff Maajar, kwa niaba ya Taasisi
ya Hassan Maajar Trust walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.
Engineer Stella Manyanya.
Shule ziliopokea madawati hayo
ni: Sopa na Mkowe (Halmashauri ya Kalambo), Korogwe na Wampembe (Halmashauri ya
Nkasi), Maleza na Mleche (Halsmashauri Sumbawanga) na shule Chipu na Kasense (Manispaa Sumbawanga).
“"Elimu ni muhimu kwa
maendeleo ya taifa letu kwa hiyo sisi tunafurahia msaada kama huu,"
alisema Mh. Mhandisi Stella Manyanya, Mkuu wa mkoa Rukwa. "Watoto wetu
wanakabiliwa na changamoto nyingi na hili la ukosefu wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia kweli lina athiri maendeleo yao. Kwa hivyo natoa shukurni nyingi
kwa Taasisi ya Hassan Maajar Trust na kazi yao hii ya kijamii ni ya kupongezwa
”, aliongeza.
Huu ni msaada wa nne chini wa
mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A
Desk For Every Child) na mkoa wa Rukwa ni mkoa wa nne kati ya mitano
itakayonufaika kwa msaada inyatolewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana
na michango iliyotolewa kufuatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011.
Hadi sasa
Hassan Maajar Trust imekabidhi jumla ya madawati 1,515 kati ya madawati 1,764;
Njombe (680), Singida (264), Mwanza (250) na sasa Rukwa (321). Mkoa utaofwatia
ni Lindi (250). Garama za madawati haya ya mkoa wa Rukwa ni jumla ya Tsh
22,500,000.
Hassan Maajar Trust pia imeshirikiana na African
Barrick Gold (ABG) kupitia Mfuko wao wa Maendeleo kutoa madawati 2,360 kwa shule 15 katika
Wilaya ya Kahama, Shinyanga yenye thamani ya dola 300,000 (takribani shilingi
milioni 480)
"Sisi kama Hassan Maajar Trust tuna
malengo ya kuboresha mazingira ya kujifunza katika shule nchini Tanzania. Kwa
kupitia kampeni yetu ya 'Dawati Kwa Kila Mtoto' tunatarajia
kufikia shule nyingi iwezekanavyo, "alisema Zena M Tenga Mkurugenzi
Mtendaji wa Hassan Maajar Trust," Na pia tunaamini kwamba mtu yeyote
anaweza kuchangia katika hii kampeni
yetu na kuchangia maendeleo ya shule zetu kwa njia ya mchango wowote mkubwa au
ndogo ", aliongeza.
huu ni mfano wa kuigwa
ReplyDelete