Walishikana mikono kuashiria ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo
Wasanii wa Tanzania House of Talent (THT) wakitumbuiza
katika uzinduzi wa kampeni ya Night Watch inayolenga kuhamasisha matumizi ya
vyandarua nyakati za usiku
Balozi wa
kujitolea wa vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria Mwasiti Almasi akimkabidhi fulana
yenye ujumbe wa mapambano ya vita dhidi ya Malaria Michael Finlay wa ExxonMobil
ambao ni wadau wakubwa wa mapambano dhid ya Malaria ( Na Mpigapicha Wetu)
Diamond alikuwapo kuwapa tafu.
Na Mwandishi
Wetu
WASANII
ambao ni mabalozi wa vita dhidi ya Malaria wametakiwa kuendeleza mapambano
dhidi ya ugonjwa huo ili kuinusuru jamii kubwa ya wanajamii.
Wito huo
ulitolewa juzi na Meneja wa Mradi wa Kitaifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) Dk
Ally Mohamed wakati akizindua kampeni mpya ya kupambana na ugonjwa wa Malaria
iitwayo Night Watch inayoratibiwa na mradi wa Zinduka na kuwashirikisha
mabalozi hao.
Dk Mohamed
alisema kuwa wasanii wanaweza kutumia nguvu ya sanaa katika kuielimisha jamii
juu ya ugonjwa wa Malaria hasa kwa kuondoa dhana potofu ambazo zinarudisha
nyuma juhudi za serikali katika kupinga ugonjwa wa Malaria.
Alisema kuwa
kampeni hiyo mpya ya Night Watch ambayo inawahamasisha wanajamii kutumia
vyandarua nyakati za usiku ni kampeni nzuri na yenye kuleta tija katika vita
dhidi ya Malaria.
Aliongeza
kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa
maambukizi ya malaria nyakati za usiku
na hivyo aliwataka wasanii hao kutumia nafasi zao katika jamii
kuhakikisha kuwa wanaitumia vema kampeni hiyo ya Nighwatch kuwakumbusha
wanajamii kutumia vyandarua na masuala mengine muhimu.
“ Mradi NMCP
unatambua mchango wa wasanii katika kupambana na ugonjwa wa Malaria ambapo
kupitia kamepni hizi zinazofanywa mmewezea kuongeza uelewa wa watu juu ya
ugonjwa huu na namna ya kupambana nao” alisema Dk Mohamed.
Wakizungumzia
kampeni hiyo wasanii Mwasiti Almasi na Fid Q alisema kuwa wakiwa kama wasanii
watatumia vipaji vyao katika kuhakikisha kuwa wanawakumbusha wanajamii umuhimu
wa kutumia vyandarua.
Fiq Q
alisema kuwa atahakikisha kuwa katika ngazi ya kifamilia wazazi na watoto
wanatumia vyandarua kila usiku ili kuweza kuepuka maambukizi dhidi ya ugonjwa
huo.
Pia hafla
hiyo ilihudhuriwa na Michael Finlay wa ExxonMobil ambao kwa pamoja na African
Barrick Gold ni wamekuwa wakidhamini shughuli mbalimbali za mapambano dhidi ya
ugonjwa wa Malaria.
Kampeni hiyo
ya Nightwatch itaanza kutangazwa katika kituo cha redio cha TBC kuanza kesho
(Jumatano) ambapo wasanii wanaoshiriki katika kampeni hiyo ni Diamond, Barnaba,
Linah, Mwasiti, Bi Kidude na Professor J.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment