Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Omari Mbura akitoa maelezo kwa waandishi kuhusiana na tukio hilo la kesho katika ukumbi wa Nkuruma, pembeni yake ni Mustapha Hasanali
Mtaalamu kutoka nchini India ambae ni mmoja kati ya waratibu wa shughuli hiyo ya kesho.
Na Mwandishi wa Elimubora
WASANII wa
muziki wa kizazi kipya Dully Sykes na Chidi Benz watasindikiza uzinduzi shindano
la wanafunzi litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu
cha Dar es salaam.
Shindano
hilo litakalozinduliwa kesho linashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini chini
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ushirikiano na mpango wa kuendeleza
wajasiriamali vijana unaodhaminiwa na serikali ya India kupitia mradi wake wa
IndiAfrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Meneja Masoko wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Mbura
Omari alisema kuwa hakutakuwa na kiingilio siku hiyo ya kesho ambapo shughuli
itaanza tangia asubuhi.
Akizungumzia
shindano hilo Mbura alisema kuna vipengele vingi ambavyo vijana
wanashindanishiwa ikiwa mojawapo ni kuangalia uelewa wao katika Nyanja za
biashara, mazingira, uchumi na nyinginezo nyingi.
Alisisitiza
kuwa utamaduni ikiwa ni moja kati ya Nyanja muhimu wanafunzi wanatakiwa
kuandika masuala muhimu ya kujadili katika Nyanja ya utamaduni.
Alisema kuwa
ili kuweza kuibuka mshindi katika shindano la hapa nchini na lile la Afrika
kiujumla wanafunzi wanatakiwa kuonesha umakini katika kutetea kile ambacho
wanaona kuwa kinafaa katika masuala ya utamaduni.
Alisema kuwa
mshindi wa jumla katika kanda ya Afrika atapata milioni kumi lakini pia
kutakuwa na mshindi wa nchi ambapo atapatikana mmoja katika kila Nyanja.
“ Katika
shindano hili vijana watashirikiana katika nyanja za uandishi wa insha, upigaji
wa picha na ubunifu katika kuwasilisha ujumbe pia lakini pia wataandika
michanganuo yao katika Nyanja mbalimbali ambapo lengo ni kuwapatia fursa ya
kuonesha uwezo wao katika kufikiri” alisema Mbura.
Katika
kusisitiza na kuonesha nia ya kuimarisha ushirikiano huo mbunifu wa mavazi
nchini Mustapha Hasanali aliahidi kusaidia mbunifu chipukizi mmoja katika wiki
ya mitindo ya Swahili ambapo ataenda kushiriki kuonesha mitindo nchini Afrika
Kusini.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment