Msanii wa muziki wa asili Chemundu Gwao akiwa na wasanii waliofanya vema katika BSS mwaka jana Haji Ramadhan na Wazzi
Chemundu Gwao akichangia mada
Mmiliki wa Bernchmark Production ambae ndio mmiliki wa program ya BSS Ritha Paulsen akisistiza jambo kwa mratibu wa BSS katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Vicky Temu.
Na Evance
Ng’ingo
BARAZA la
Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii waliotoka katika mradi wa Bongo Star
Search kuwa na mikakati ya kujiendeleza wenyewe badala ya kutegemea kusaidiwa
na mradi huo pindi shindano linapokwisha.
Wito huo
ulitolewa jana na mratibu wa BSS katika Basata Vicky Temu wakati akichangia
mada katika mkutano uliowashirikisha BSS na wadau wa sanaa na kufanyika Basata.
Vicky
alisema kuwa wasanii hao wanatakiwa kutambua kuwa uhusiano kati ya BSS na
wasanii hao unamalizika mara baada ya shindano hivyo wanatakiwa kutumia vema
elimu ya muziki waliyoipata wakiwa ndani ya shindano hilo kujiendeleza zaidi.
Hata hivyo
alimtaka mwandaaji wa shindano hilo Ritha Paulsen kuwaendeleza wasanii hao ikiwa
pamoja na kuingia mkataba na studio za kurekodia muziki kwa lengo la
kuwaendeleza zaidi watakaofanya vema pindi shindano linapomalizika.
Wakati huo
huo mwandaaji wa shindano hilo Rita, aliwataka waandishi pamoja na watangazaji
wa redio na luninga kuwasaidia wasanii watokao katika BSS badala ya kuwakatisha
tama.
Alisema kuwa
kuna wadau mbalimbali katika vyombo vya habari na sanaa kiujumla ambapo
wanawakatisha tamaa wasanii watokanao na mradi wa BSS kwa kutotaka kuwasaidia
kuwatangaza.
Katika hatua
nyingine gazeti hili lilishuhudia hali ya mtafaruku katika ya Rita na BSS
katika suala la upatikanaji wa kibali cha mwaka huu na suala la upangaji wa
majaji.
Rita
alilalamikia kitendo cha Basata kutaka kumpatia kibali cha muda cha kuandaa
shindano hilo kwa mwaka huu mpaka pale atakapomweka bayana mdhamini wake wa
mwaka huu huku Rita akisisitiza kuwa apewe kibali kamili ili mdhamini wake
aweze kusaini mkataba kwa kuwandio atakuwa na imani kuwa shindano lipo.
“ Sasa
mkinipa kibali kamili si ndio mdhamini atatoa huo udhamini na kutuhakikishia
kuwa anatudhamini kwa mwaka huu au? Mkinipa kibali cha kawaida ntashindwa
kupata udhamini kwa nini kwanza msinipe kibali cha mwaka mzima” alihoji Rita.
Kwa upande
wake Kaimu Mwenyekiti wa Kitengo cha Matukio cha Basata, Malimu Mashili alisema
kuwa baraza hilo haliwezi kutoa kibali kamili kabla halijapata mwelekeo wa
shindano la mwaka huu ili kwa kuwa chochote kikiharibika ni baraza ndio
litahusika.
Kikao
kilimalizika huku Basata ikiwa imemtaka Rita kuwasilisha bajeti inayotaja
zawadi, na gharama nyinginezo licha ya kuwa Rita aliwataka wampatie kibali
kamili ili aweze kusaini mkataba na mdhamini wake lakini hata hivyo alisema
kuwa suala la kutaja zawadi ni mapema mno kwa kuwa wadhamini wengine hujitokeza
shindano likiwa limenza.
Mtafaruku
mwingine uliibuka katika suala la upatikanaji wa majaji wa shindano hilo ambapo
Basata ilimtaka Rita kuwapelekea majina ya watu watano ili iweze kuwachagua
watatu kati yao huku ikisisitiza kuwa huo ni utaratibu wa kawaida.
Akionesha
kushangazwa na utaratibu huo Rita alisema kuwa anapenda kuwatumia majaji wake
wale wale kwa kuwa ndio ameshawajengea hisiza nzuri kwa washabiki wa BSS na
huvuti kipindi hivyo kuwabadilisha sio haki.
Mkutano huo
ulivuta hisia za wadau mbalimbali wa
sanaa waliokuwa katika mkutano huo uliodumu kwa saa tatu kwa lengo la
kutathmini maendeleo ya BSS, lakini hata hivyo Basata ilimpongeza kwa kuendesha
shindano hilo kwa miaka sita bila ya kusimama.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment