WADAU wa
elimu wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali zinazopelekea wanafunzi kushindwa
kufanya vema katika masomo pamoja na mitihani yao ya mwisho.
Ukosefu wa
vitabu ni moja kati ya sababu za msingi ambazo zinasababisha wanafunzi
kushindwa kufanya vema katika masomo yao.
Licha ya serikali kupitia wizara ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoa ruzuku kwa shule mbalimbali za
serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari lakini bado hali sio shwari katika
upatikanaji wa vitabu hivyo.
Ukosekanaji
wa vitabu hivyo unasababaishwa na sababu mbalimbali moja wapo ikiwa ni
mazingira tata ya upatikanaji wa tenda za kununulia vitabu hivyo.
Kuna tetesi
kuwa wakuu wa shule ndio hutoa fedha za kununulia vitabu hivyo na hivyo kuwa
katika mazingira ya kuwapatia tenda watu wao wa karibu na pengine wasiokidhi
vigezo vya kupewa tenda hizo.
Matokeo yake
watu hao huishia kununua vitabu pungufu na pengine kununua vitabu ambavyo
haviendani na muda au mahitaji husika.
Mmiliki wa
maktaba ya uuzaji wa vitabu ya Salamanda Clarence Mponda anasema kuwa awali wakati
zabuni zikitolewa na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi mfumo wa upatikanaji
wa zabuni ulikuwa upo wazi na wa kuridhisha.
Anasema kuwa ilikuwa ni rahisi kwa
wazabuni wadogo pia kupata nafasi za kusambaza vitabu kwa kuwa walikuwa
wakishindana.
Anasema kuwa
kwa sasa suala la manunuzi ya vitabu lipo chini ya Tamisemi na kuongeza kuwa
walimu wakuu wanakuwa na nguvu zaidi katika kununua vitavbu hivyo.
Anasema kuwa
hali hiyo inaleta utata kwa kuwa mfumo wa upatikanaji wa zabuni sio wa wazi
tena na inawawia vigumu wao kama wanunuzi wa vitabu kupata tenda za kununua
vitabu hivyo.
“ Ni kwamba
yani kwa sasa huu utaratibu ni kama vile sio mzuri kwa kuwa zamani ilikuwa
rahisi mno sisi tulikuwa tunaenda moja kwa moja kugombania tenda katika
Halmashauri za wilayani na mambo yalikuwa yanaenda vema sana” alisema Mponda.
Hata hivyo
ofisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Lucy Gurtu anapingana na hoja hiyo kwa
kufafanua kuwa kwa kawaida walimu wakuu hawana idhini ya kununua vitabu moja
kwa moja.
Anasema kuwa
fedha za ruzuku za vitabu zinapotoka Tamisemi hufika kwanza katika ofisi ya
wilaya na kisha kupangiwa matumizi kulingana na mahitaji ya shule husika.
Anasema kuwa
kupitia wakaguzi wa elimu wa wilaya ofisi yake hugundua shule yenye uhaba wa
vitabu na kuchanganua ni vitabu vya aina gani vinahitajika kwa muda huo.
Anasema kuwa
pia walimu wenyewe hupeleka maombi kwa ofisa elimu wa wilaya kuelezea mahitaji
halisi ya vitabu vinavyotakiwa.
Anasema kuwa
kutokana na hilo kunakuwa hakuna mianya ya rushwa kwa kuwa walimu wakuu
wanajengea hoja ya hitaji husika na kuliombea fedha.
Anasema kuwa
wakuu wa shule huandika idadi ya vitabu inavyohitaji kwa kuchanganua ni vya
aina gani na pia hata kama wakihitaji vifaa vya mahabara pia hutoa mapendekezo
ya aina ya vifaa.
Anasema kuwa
baada ya kutoa mchanganuo ofisi yake huwapatia fedha za kununulia vitabu husika
na hivyo walimu hununua vitabu kulingana na mahitaji waliyohidhinisha.
Anasema kuwa
iwapo walimu ikibainika kuwa hawakununua vitabu kulingana na makubaliano husika
wakaguzi wa elimu wanalo jukumu la kuwachukulia hatua.
Anasema kuwa
wakaguzi wa elimu kwa kushirikiana na wakaguzi wa ndani wa Manispaa huendesha
zoezi la ukaguzi na kutoa ripoti kuhusiana na manunuzi ya vitabu husika.
“ Ni kwamba
najua yani kunakuwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa pamoja inatakiwa
kushirikiana katika kuzitatua, mfano suala la kuwa na wakaguzi wa kutosha wa
kukimbia huku na huko kukagua masuala muhimu ya elimu katika wilaya na
mengineo” anasema Lucy.
Kutokana na
hakli hiyo ya wakuu wa mikoa kupewa fedha za kununulia vitabu kulingana na
mahitaji yao huenda ndilo linalopelekea mazingira ya rushwa katika kutoa zabuni
hizo.
Naibu Katibu
Mkuu wa ofisi ya waziri mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jumanne
Sajni anafafanua zaidi kuwa ofisi yake hupeleka fedha kwa ofisi za elimu za
wilaya ambazo ndio huwa na jukumu la kununua vitabu.
Anasema kuwa walimu huwa na jukumu la
kuidhinisha aina ya vitabu vya kununuliwa na kisha kupelekea maombi sehemu husika
na pia ufuatiliaji wake hufanyika kiundani ili kuhakikisha kuwa vitabu
vimenunuliwa.
“ Mimi
ninchoweza kusema kuwa kama kuna walimu ambao wanachakachua ununuzi wa vitabu
basi ni jukumu la kamati ya shule kuhakikisha kuwa linashughulikia suala hilo”
alisema Sajni.
Alisema kuwa
Mkuu wa shule husika anajadiliana na kamati ya shule katika kuamua aina ya
vitabu vya kununua na
kisha kuanza kwa pamoja mchakato wa kununua vitabu hivyo.
kisha kuanza kwa pamoja mchakato wa kununua vitabu hivyo.
Lakini hata
hivyo alikiri kuwa huenda kukawepo kwa dalili za mazingira hayo ya rushwa na
hivyo alitoa wito kwa maofisa wa elimu wa wilaya kushirikiana na maofisa ugavi
na wakaguzi wa elimu kufuatilia manunuzi ya vitabu.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment