KAMATI
inayoshughulikia vazi la taifa imeeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya
mchakato wa kutafuta vazi hilo.
Akizungumza
katika mkutano na wadau wa sanaa ya ubunifu Mwenyekiti wa kamati ya vazi la
taifa Ndesamburo Merinyo alisema kuwa wadau wengi wamejitokeza kufanikisha
upatikanaji wa vazi hilo.
Merinyo
alisema kuwa wadau hao ni pamoja na wachoraji wa michoro ya mavazi na pamoja wa wadau wengine.
Alisema kuwa
kwa sasa wamepata michoro mingi kutoka kwa wachoraji mbalimbali ambao wamekuwa
wakielezea namna amabcho kitambaa cha vazi la taifa kinatakiwa kuwa.
Alisema kuwa
kabla ya kupatikana kwa vazi la taifa kwanza kunakuwa na kitambaa cha vazi hilo
ambacho ndio kitatumika kupata vazi lenyewe.
Alisema kuwa tayari kamati yake imeendesha
midahalo mbalimbali ikiwashirikisha wadau wa ubunifu, mavazi na sanaa kiujumla
na tayari imekusanya mawazo yao kuhusiana na vazi hilo.
“ Ni kwamba
kwa sisi kama kamati tunaona kuwa zoezi hili litakuwa ni lenye mafanikio
makubwa kwa kuwa mwamko kutoka kwa watanzania ni mkubwa na safari hii kazi
takamilika kama ilivyopangwa” alisema Merinyo.
Kamati ya
vazi la taifa iliundwa mapema mwaka huu na waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana
na Michezo Emanuel Nchimbi kwa lengo la kutafuta vazi la taifa litakalotambulisha
taifa la Tanzania.
Katika
mdahalo huo wa basata wadau mbalimbali walitoa mawazo yao kuhusiana na
wanavyotaka kitambaa hicho kuwa
Mwisho
0 comments:
Post a Comment