Wakitumia sanaa za maonesho kutoa ujumbe wa Malaria
Waelimishaji wakiwauliza maswali watoto hao
Na Evance
Ng’ingo
KUNDI la
Tanzania House of Talent (THT) limeanza ziara ya siku 60 kwa mikoa ya kanda ya
Ziwa ambapo wanatumia sanaa ya maonesho kuelimisha kuhusu ugonjwa wa Malaria.
Ziara hiyo
inahusisha mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera na
Shinyanga ambapo wasanii hao wanafika mpaka wilaya za vijijini
kuelimisha wanafunzi na wanajamii juu ya ugonjwa huo.
Akizungumzia
ziara hiyo meneja wa mradi wa Zinduka unaoratibu zoezi hilo, Sadaka Gandi
alisema wasanii wanane wapo katika msafara huo.
Alisema kuwa
wasanii hao watatumia snaaa ya maigizo, nyimbo pamoja na muziki wa asili katika
kufikisha ujumbe.
Alisema kuwa
kwa kutumia sanaa THT imeweza kuifikia idadi kubwa ya wanajamii na kufanikiwa
kuwaelimisha juu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria na namna ya kujikinga nao.
Alisema kuwa
ziara hiyo inatarajiwa kumalizika machi 22 mwaka huu baada ya kuzungukia mikoa
yote na kutoa elimu husika ya malaria.
“ Kupitia
mradi huu wa utoaji wa elimu ya Malaria kwa njia ya sanaa wasanii wameweza
kulifanikisha zoezi hili kwa hali ya juu kwa kuongeza hamasa ya wananchi katika
kushiriki vita dhidi ya ugonjwa huu” alisema Sadaka.
Zaiara ya wasanii
hao imeanzia na mkoani Mara ambapo
wametembelea shule mbalimbali za sekondari na kuanzisha klabu za wanafunzi zenye
majukumu ya kupambana na ugonjwa wa
Malaria.
Wasanii wa
THT waliopo katika ziara hiyo ni wale wanaojishughulisha na uchezaji wa aina
mbalimbali za ngoma na kuimba.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment