Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi aliyekuwa akimwelezea changamoto mbalimbali walizonazo shuleni hapo.(Picha na Zainul Mzige).
Na MOblog, Shinyanga
SHULE ya watoto wenye ulemavu ya Buhangija Jumuishi inakabiliwa na changamoto kubwa zinazofanya maisha kwa watoto hao kuwa magumu.
Miongoni mwa changamoto hizo ni kukosekana kwa huduma za matibabu, walimu wa kutosha na mabweni.
Hayo yamebainika wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi, ndiye aliyeelezea ugumu uliopo katika shule hiyo yenye wanafunzi 209 wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanyia ziara fupi akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (katikati).
Alisema shule hiyo yenye walemavu wa aina tatu wa kusikia, ngozi na wasioona inakabiliwa pia na lishe duni ambayo haimpi kijana nafasi ya kuendelea, kwani wanakula mlo wa aina moja na kidogo.
Shule hiyo ambayo awali ilikuwa inawapokea wanafunzi wasioona sasa inapokea walemavu wa ngozi kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
Aidha mwalimu huyo alisema kwamba wameiomba serikali kuwa na muuguzi na daktari katika makazi hayo lakini mpaka sasa hawajapatiwa kutokana na wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuwalipa.
Alisema kutokana na rika mbalimbali na tatizo la walemavu wa ngozi shule hiyo ambayo sasa imegeuzwa kuwa makazi inastahili kuwa na daktari na mabweni yaongezwe.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ( wa pili kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga (hawapo pichani) alipofanya ziara fupi akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (wa pili kulia). Kulia ni Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.
Aidha mwalimu alisema walimu kwa ajili ya viziwi hawatoshi.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, amesema ameyaona mazingira hayo na kuahidi kushirikiana na marafiki na mamlaka nyingine kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Alisema kwamba amefurahishwa kuwapo katika kituo hicho na kuona namna wanavyoweza kusaidia sehemu hiyo ya jamii kutojisikia upweke.
Akizungumza na watoto hao walimwambia kwamba wana changamoto ya nguo, vitanda, vitabu na mahitaji mengine ya lazima kama watoto na wanafunzi.
Baadhi ya watoto wanaosoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani).
Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Loreto mkoani Shinyanga Beatrice Leme anayelelewa kwenye kituo hicho kutokana na kukithiri kwa mauaji ya walemavu wa ngozi mkoani humo akimwelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa niaba ya wanafunzi wenzake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanya ziara fupi shuleni hapo.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga, Daniel Limbu akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias pamoja na Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi wakifurahi pamoja na watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule hiyo.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo hicho ambacho ni salama kwao kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
Baadhi ya majengo ya mabweni ya shule ya msingi Buhangija ya wilayani Shinyanga.
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakicheza mpira kwenye mazingira salama shuleni hapo kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha mtoto Erick mwenye ulemavu wa ngozi kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyefanya ziara fupi kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu (mahitaji maalum).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsuka kwenye bembea mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi Zawadi Deus anayesoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga wakati wa michezo alipofanya ziara fupi shuleni hapo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni wakati akijiandaa kuondoka shuleni hapo baada ya kuhitimisha ziara yake fupi. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.
KAWAIDA
0 comments:
Post a Comment