Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza maelezo kuhusu shule ya Sekondari Mburahati mara baada ya kuzuru shuleni hapo.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato akielezea changamoto zinazoikabili shule hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzuru shule ya Sekondari Mburahati .Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) akimsikiliza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato akitoa maelezo kuhusu kukwama kwa ujenzi wa madara ya shule ya Sekondari Mburahati mara baada ya kuzuru shuleni hapo, Mwingine ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James mkubo.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mburahati
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumatano, Mei 24, 2017
ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg
John Lipesi Kayombo kuanza mchakato wa ukamilisho wa ujenzi wa Madarasa
manne katika shule ya Sekondari Mburahati iliyopo Katika Mtaa wa Barafu,
Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam.
Sambamba na Agizo hilo pia ameagiza kujengwa vyoo vya wanafunzi kutokana
na uchache wa vyoo vilivyopo ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo wakati wa kikao Cha pamoja
kilichofanyika Shuleni hapo kwa kuhudhuriwa na Uongozi wa Shule hiyo,
Kamati ya Shule, Uongozi wa serikali ya Mtaa na Afisa Mtendaji wa Kata
ya Mburahati.
Mhe Makori alisema kuwa kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na
kidato Cha kwanza Kila mwaka kumekuwa na upungufu mkubwa wa madawati
Jambo ambalo linachangia wanafunzi shuleni hapo kuanza kusoma kwa
kupokezana hivyo mpango mahususi kukabiliana na changamoto hiyo ni
pamoja na kuanza kujenga miundombinu ya kutosha itakayowasaidia
wanafunzi kupata elimu bora.
Akizungumzia changamoto ya upungufu wa walimu shuleni hapo Mkuu wa
Wilaya alisema kuwa wakati serikali inajiandaa na mkakati wa jumla wa
kuikabili changamoto hiyo ni vyema uongozi wa shule kutafuta walimu wa
muda ili kupunguza kadhia ya wanafunzi kukosa vipindi kwa sababu ya
upungufu wa walimu.
Shule ya Sekondari Mburahati ni shule ya kutwa iliyoanzishwa mwaka 2010
ambapo pamoja na kuwa na wanafunzi wengi ina jumla ya vyumba vya
madarasa 9 huku mahitaji yakiwa ni vyumba 25 hivyo kupelekea kuwa na
upungufu wa madarasa 16.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Mhe Makori amesema kuwa pamoja na changamoto
nyingi zinazoikabili shule hiyo lakini Manispaa ianze na changamoto za
utatuzi wa Uhaba wa Madarasa na upatikanaji wa vyoo vya kisasa.
Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Walimu wenzake, Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato amempongeza Mkuu wa
Wilaya ya Ubungo kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo utatuzi wa migogoro
ya Ardhi na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Wilaya hiyo.
Kashato ametumia nafasi hiyo pia kumuomba Mkuu huyo wa Wilaya kusaidia
utatuzi wa changamoto ya Upungufu wa vitabu vya kufundishia masomo ya
sanaa kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi, Kukamilishwa Mfumo wa gesi
katika Maabara ya shule hiyo na ujenzi kwa ajili ya jengo la Utawala.
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo
Click here to Reply, Reply to all, or Forward
|
0 comments:
Post a Comment