Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, July 31, 2017

PiMAK yafungua duka Dar

Mmiliki wa kampuni hiyo, Riza Ergun akiwa na wadau kadhaa waliojitokeza kwenye uzinduzi huo

Wafanyakazi na wageni waliojitokeza siku hiyo ya uzinduzi wa duka



Riza Erguna akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka lake hilo hapa nchini

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya kimataifa inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya mbalimbali vya mapishi kwenye hoteli , PiMAK  imefungua duka hapa nchini lililopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.


Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez alisema, kampuni hiyo imebainisha soko kubwa la bidhaa zake hapa ambapo imekuwa ikifanya biashara kwa muda mrefu kwa kushirikiana na mawakala, na kwa sasa licha ya kufungua duka hilo lakini bado inaona kuna fursa kubwa zaidi za uwekezaji.

Akizungumzia kuhusiana na bidhaa hizo, alisema kuwa ni bidhaa kwa ajili ya matumizi ya hoteli, migahawa na huduma kubwa za mapishi vikiwamo vya kukatia nyama, kuhokea mikate, kuoshea vyombo, kupikia na huduma nyingine za kihoteli.


Aliongeza kampuni hiyo imeshafanya kazi hapa nchini kwa miaka minne ikishirikiana na mawakala ambapo vifaa hivyo vinatumiwa na hoteli nyingi hapa nchini, huku akiweka wazi kuwa inatoa huduma za utengenezaji wa bidhaa hizo pia.


"Kampuni hii ina miaka 25 na makao yake makuu ni Instabul, Uturuki kwa Tanzania tumekuwapo kwa miaka minne tukifanya biashara kwa kushirikiana na mawakala lakini leo tumefungua (jana) tumefungau duka letu huku tukiwa na lengo na kuja kuanzisha kiwanda cha uundwaji wa vifaa hivi hapa hapa nchini" alisema Donmez.



Pia alisema kuwa kampuni hiyo kwa miaka ya baadae itafungua kiwanda hapa nchini kwa lengo la kurahisha upatikanaji wa bidhaa zake kwenye soko la Afrika Mashariki na Kati na pia kuongeza ajira zaidi kwa watanzania.

Kampuni hiyo kwa sasa inafanya kazi nchi 16 na kwa hapa nchini imeshaajiria wafanyakazi 15 huku ikitoa huduma za ukarabati wa vifaa vya upishi hoteli mbalimbali nchini.
==============================================

Wednesday, May 24, 2017

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AAGIZA KUANZA UJENZI WA MADARASA MANNE NA VYOO VYA SHULE YA SEKONDARI MBURAHATI


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika shule ya Sekondari Mburahati iliyopo Katika Mtaa wa Barafu, Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza maelezo kuhusu shule ya Sekondari Mburahati mara baada ya kuzuru shuleni hapo.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato akielezea changamoto zinazoikabili shule hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzuru  shule ya Sekondari Mburahati .Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) akimsikiliza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato akitoa maelezo kuhusu  kukwama kwa ujenzi wa madara ya shule ya Sekondari Mburahati mara baada ya kuzuru shuleni hapo, Mwingine ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James mkubo.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mburahati



Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumatano, Mei 24, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza mchakato wa ukamilisho wa ujenzi wa Madarasa manne katika shule ya Sekondari Mburahati iliyopo Katika Mtaa wa Barafu, Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam.
Sambamba na Agizo hilo pia ameagiza kujengwa vyoo vya wanafunzi kutokana na uchache wa vyoo vilivyopo ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo wakati wa kikao Cha pamoja kilichofanyika Shuleni hapo kwa kuhudhuriwa na Uongozi wa Shule hiyo, Kamati ya Shule, Uongozi wa serikali ya Mtaa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mburahati.
Mhe Makori alisema kuwa kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha kwanza Kila mwaka kumekuwa na upungufu mkubwa wa madawati Jambo ambalo linachangia wanafunzi shuleni hapo kuanza kusoma kwa kupokezana hivyo mpango mahususi kukabiliana na changamoto hiyo ni pamoja na kuanza kujenga miundombinu ya kutosha itakayowasaidia wanafunzi kupata elimu bora.
Akizungumzia changamoto ya upungufu wa walimu shuleni hapo Mkuu wa Wilaya alisema kuwa wakati serikali inajiandaa na mkakati wa jumla wa kuikabili changamoto hiyo ni vyema uongozi wa shule kutafuta walimu wa muda ili kupunguza kadhia ya wanafunzi kukosa vipindi kwa sababu ya upungufu wa walimu.
Shule ya Sekondari Mburahati ni shule ya kutwa iliyoanzishwa mwaka 2010 ambapo pamoja na kuwa na wanafunzi wengi ina jumla ya vyumba vya madarasa 9 huku mahitaji yakiwa ni vyumba 25 hivyo kupelekea kuwa na upungufu wa madarasa 16.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Mhe Makori amesema kuwa pamoja na changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo lakini Manispaa ianze na changamoto za utatuzi wa Uhaba wa Madarasa na upatikanaji wa vyoo vya kisasa.
Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Walimu wenzake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo utatuzi wa migogoro ya Ardhi na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Wilaya hiyo.
Kashato ametumia nafasi hiyo pia kumuomba Mkuu huyo wa Wilaya kusaidia utatuzi wa changamoto ya Upungufu wa vitabu vya kufundishia masomo ya sanaa kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi, Kukamilishwa Mfumo wa gesi katika Maabara ya shule hiyo na ujenzi kwa ajili ya jengo la Utawala.
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo

Monday, May 22, 2017

Rambirambi za waliopoteza maisha St Vicent zazidi kutolewa

 Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja  Kanda ya kaskazini  Deipyen Bameda  (TASDOA ) katikati ni Katibu mkuu  TASDOA Tinno Mmasi akiwa anafafanua jambo mara baada ya kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Rambirambi zao za vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent
 Dare salaam Independent School (DIS) Anna Msangi akiwa anakabidhi kiasi cha shilingi milioni tatu kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni mchango wao kwa wanafunzi wa Lucky Vicent
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifafanua jambo ofisini kwake kabla ajapokea rambirambi hizo

Habari picha na  Woinde Shizza,Arusha

Baadhi ya  Wanasiasa  wametakiwa kuacha  mara moja kuchulia tukio la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kama sehemu yao ya kujinufaisha  kisiasa, pamoja na baadhi yao kupotosha jamii kupitia  mitandao ya kijamii .

Hayo yamebainishwa jana  na mkuu wa mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo wakati alipokuwa akipokea rambirambi za wanafunzi  32 wa Lucky Vicent,zilizotolewa na chama  cha wamiliki  wauza mafuta rejareja (TASDOA) pamoja  na uongozi wa shule binafsi ya Dare salaam Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea umaarufu.


Alisema kuwa swala hili sio tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamoto kubwa iliyozikumba familia za wananchi wa Arusha ,hivyo linatakiwa kuheshimika na kuchukuliwa kama ni tatizo kubwa lililowakumba wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani kuwapoteza watoto hawa ni jambo  la kusikitisha sana kwani walikuwa wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.

“pia napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuleta michango yenu kwa ajili ya wanafunzi hawa 32 ila napenda pia kuwakumbusha kuwa  jumla ya watu wote waliopata tatizo walikuwa 38 lakini kati yao waliokufa ni 35 na  na wingine watatu ni majeruhi hivyo napenda kuwasihi wananchi na mashirika ambayo wanaleta msaada wasiangalie waliopoteza maisha tu bali wawakumbuke na wale majeruhi watatu ambao wapo nje kwa matibabu kwani wao pia ni binadamu”alisema Gambo

Alisema kuwa japo kuwa majeruhi wale waliopelekwa nje kutibiwa wanaudumiwa bure lakini kuna wale watu ambao wameenda nao pamoja ya kuwa wanahudumiwa chakula na malazi lakini kwa binadamu waka waida anatakiwa kujitegemea kwa vitu vidogovidogo hivyo ni vizuri kama watu wanaotoa msaada wata wakumbuka na hawa majeruhi .

Kwa upande wake katibu mku u wa  chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) Tino Mmasi alisema kuwa wao kama wamiliki wawauza mafuta wadogowadogo wameguswa sana na msiba huu na ndio maana walioamua kukaa kama wanachama na kuchanga fedha hizi kiasi cha shilingi millioni saba laki saba  ili ziwafariji wafiwa hawa 35 na pia wameaidi kwend a kujichanga tena  kwa ajili ya kuwachangia majeruhi ambao wapo Marekani

“tumetoa hiki kidogo lakini kwa jinsi  tulivyoguswa tutaenda kuchanga fedha zingine kwa ajili ya majeruhi waliopo marekani na tunapenda kukuaidi mkuu wa mkoa tutakuwa nanyi bega kwa bega hadi majeruhi hawa wote wapone na warudi hapa nchini”alisema  Mmasi

Katika michango hii shule ya  shule binafsi ya Dare salaam Independent School (DIS) ilichanga kiasi cha shilingi  milioni tatu  laki moja na nusu  huku chama cha wamiliki wa uzamafuta rejareja wakiwa wamechangia shilingi milioni saba laki saba  huku wote wakiaidi kwenda kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya majeruhi.

Sunday, May 21, 2017

Camara Education Tanzania yaendelea kuwanoa wanafunzi


Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na uwezeshaji wa elimu kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Tehama, Julia Pierre-nina akiwaelekeza jambo walimu kutokea shule mbalimbali namna bora ya matumizi ya Tehama, pembeni yake ni Mkuu wa Mauzo na Masoko, Adam Kawa (Picha na Evance Ng’ingo)