Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, November 22, 2015

NYAKOREMA RIOBA donates books to READ International

Nyakorema Rioba left, giving a book to a Read representative
 




Nyakorema Rioba delivered a donation of her new book ‘Nitakuwa Mfano’ (I will be a role model) to READ International on Friday 20 November. 

 Her books will be placed to new libraries that READ will be setting up in 2016 in Mtwara, Ruvuma, and Dar-es-Salaam.


Nyakorema is a mother of 2 and a female engineer working at the Tanzania Bureau of Standards, with an interest in community development, particularly youth.  

Nyakorema decided to write this book after learning that secondary schools students are only taught how to answer questions in exams, but they are not taught how to handle and solve their own pressing issues in their community and became the change they would wish to see in their community and world. 
This book encourages teenagers to develop a sense of vision and achieve their dreams.  It tells stories of other successful men and women who went through hardship but made it through and they are inspirational.

Tuesday, November 3, 2015

Mdau wa Mitindo Deo atoa somo kwa models wa Black fox


 

Na Mwandishi Wetu
VIJANA wanaojifunza fani ya Uanamitindo hapa nchini wametakiwa kutumia muda wao mwingi kujifunza fani hiyo kutoka kwa wanamitindo wenzao wa nje ya nchi.

Wito huo ulitolewa juzi na mdau wa fani hiyo ambae ni mtangazaji wa kipindi cha Nirvana kinachorushwa na kituo cha Luninga cha East Afrika, Deogratius Chitama wakati akizungumza na vijana wanaojifunza fani hiyo.

Deo alisema kuwa kutokana na ugeni wa fani hiyo hapa nchini vijana wanaotakiwa kujiajili katika fani hiyo wanayo kila sababu ya kuwafuatilia wanamitindo wakubwa wa nje ya nchi kwa kuwa wao wameshaendelea.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo itawaongezea hamasa kubwa katika kujua mengi kuhusiana na fani hiyo kuanzia uendeshwaji wake hadi fursa zilizopo katika fani hiyo.

"Ukweli ni kwamba kwa hapa kwetu hii ni moja kati ya fani mpya kabisa kwa kuwa kwanza watu wengi bado wanadhani kazi kubwa ya uanamitindo ni kuonesha mavazi tu ila kuna mengi zaidi ya hapo" alisema Deo.

Aliongeza kuwa " kwa upande mwengine hii ni fani ambayo mtu unaweza kuitumia vema ukajikuta unapata kazi za kufanya matangazo ya biashara ikiwa pamoja na kuwa balozi wa kitu fulani na hivyo hata kipato kikaongezeka".

Alisema kuwa pia ni fani ambayo inachangamoto nyingi na inatakiwa kwa wahusika kukabiliana nazo huku akiwasihi zaidi kuwa kikubwa wanachotakiwa kufanya ni kuwa na nidhamu na unyenyekevu. 

Vijana hao zaidi ya 15 wanafundishwa fani hiyo na kampuni ya Black Fox Models kila Jumapili katika mgahawa wa Paparazi uliopo Sleep way Masaki.

Mmilikiwa kampuni hiyo AJ Mynah alisema kuwa vijana wengi kwa sasa hapa nchini wamekuwa na hamasa ya kujihusisha na kazi mbalimbali zitokanazo na fani ya uanamitindo.

Alisema kuwa kikwazo kikubwa ni wengine kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na fani hiyo hasa kuanzia elimu yake kwa ujumla hadi namna ya kuifanya kazi yenyewe.

"Najua kumekuwa na mtazamo kuwa wanamitindo ni watu fulani wembamba, warefu na wazuri sana ila kumbe inawezekana hata ukawa wa kawaida ila ukawa na kitu fulani katika mwili wako ambacho unaweza kujivunia na kikatumika hata katika matangazo mfano mtu anakuwa na macho, au mdomo au hata kitu chochote ambazo anaweza kutumia kutangaza" alisema AJ.
===========

Friday, October 23, 2015

KIU kuwaokoa vijana dhidi ya dawa za kulevya

Mafunzo yakiendelea kutoka KIU



Mtaalamu akitoa somo






Na Evance Ng'ingo
SUALA la dawa za kulevya linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha ambapo serikali pamoja na wadau wengine kadhaa wamekuwa wakipambana katika kuhakikisha kuwa wanalitokomeza janga hilo.

Wadau mbalimbali wamekuwa wakiendeleza mapambano dhidi ya janga hilo kwa kutumia njia mbalimbali ambazo zinalenga kuondoa kabisa matumizi ya dawa za kulevya.

Licha ya juhudi hizo za wadau lakini bado kazi imekuwa ni ngumu katikakutimiza azma hiyo.
Chuo Kikuu cha Kampala, KIU, kimeliona tatizo hilo ambapo chenyewe kimeamua kuwasaidia wale ambao wameshaathirika na dawa hizo za kulevya.

Uamuzi huo unalenga kuwarejesha tena kwenye jamii wale ambao wameathiriwa na dawa za kulevya ambao jamii inaonekana kuwatenga.

Jamii imekuwa ikiwatenga waathirika wa dawa za kulevya na mwisho wa siku waathirika hao wamekuwa wakikosa msaada na kujikuta wakiendelea kujihusisha na dawa hizo.

Familia nyingi zimekuwa zikiona aibu kuwahifadhi waathirika wa dawa hizo na mwishoe wanaonekana kuwatenga hasa kwa kuwafukuza majumbani au kuwapeleka katika vituo vya kuhifadhia vijana waathirika wa dawa hizo.

Dhana hiyo ya familia kuona aibu katika kuwasaidia waathirika kwa dawa hizo ndio imepelekea chuo cha KIU kuanzidha kampeni ya End Shame, ikiwa na nia ya kumaliza aibu kuanzia ngazi za kifamilia hadi katika jamii.

Kumaliza huko aibu kunahusisha kwanza wanajamii wenyewe kuepuke suala la kuona aibu kushugulika na waathirika wa dawa hizo lakini pia hata kwa watumiaji wenyewe kuepuka aibu ya matumizi ya dawa hizo pia.

Aibu ambayo familia inaona kuwa imepata kutokana na matumizi ya dawa hizo za kulevya ndio imepelekea kuwapo kwa hali ya kuwasusa vijana wengi na kuwapeleka katika vituo vya kusaidia waathirika ambapo nako hali ni sio ya kuridhisha.

Wakiwa katika vituo hivyo vijana hao wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha harakati za vijana hao kurejeshwa kwenye maisha yao ya kawaida.

Chuo Kikuu, KIU katika kuliona hilo kimeamua kuingia kiundani zaidi kukabiliana na changamoto hiyo ya ukosefu wa utaalamu katika kuwahudumia waathirika hao.

Kiu imeanza kwa kuwachuja wanafunzi wake sita wanaosoma kozi Ustawi wa  Jamii chuoni hapo na kuwawezesha kuanza kufanya kazi za kujitolea katika vituo mbalimbali vya  vya kusaidia watu walioathiriwa na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi hao sita ni Cecilia Mihayo, Zenah Msuya, Florah Rafael, Clarence Lihundi, Rossie Kasanga, Clara Nahum.

Mratibu wa mpango huo chuoni hapo, Lauren Schmidt anasema kuwa mpango huo unalenga kutoa mchango wa chuo hicho katika kupambana na dawa za kulevya.

Anasema kuwa watakuwa na jukumu la kuwaelekeza vijana njia mbadala za kujitoa katika matumizi ya dawa hizo pamoja na kuwawaunganisha vijana hao na wenzao wengine ambao wameshaacha kutumia dawa hizo.

Anaongeza kuwa wanafunzi hao ni sehemu ya mkakati wa chuo hicho wa kujitoa katika kuwaihudumia jamii ya kitanzania chini ya mradi wake wa Center for Wellness and Social Innovation.

Anaongeza kuwa wanafunzi hao wameundishwa njia mbalimbali za kusaidia jamii kuanzia ushauri hadi masuala mengine muhimu katika jamii.

Anaongeza kuwa wameunganishwa na vituo mbalimbali vinavyosaidia watu walioathiriwa na dawa za kulevya na watafanya kazi kwa kushirikiana na watu wa vituoni humo.

Lakini pia anabainisha kuwa ni wakati mwafaka pia kwa wanafunzi hao nao kujifunza mengi zaidi kuhusiana na namna ya kukabiliana na dawa hizo pamoja na kujifunza kiundani zaidi tabia na sababu vijana kujihusisha na dawa hizo.

Anafafanua kuwa huo ni mradi endelevu ambapo utadumu kwa miaka mingi ijayo na unalenga zaidi kuwasaidia waathirika wanawake.

"Sisi chuo cha KIU tumeamua kuanzisha harakati za kukabiliana na mambo mengi ambayo ni mabaya katika jamii yani yale ambayo yanaathiri mustakabali wa maendeleo ya jamii ya kitanzania na hizi ni jitihada endelevu".

Anaongeza kuwa "mradi huu pia utatoa jicho la kipekee kwa wanawake walioathiriwa na dawa za kulevya ambao wengi wao wamekuwa hawapewi kipaumbele kabisa katika mapambano dhidi ya janga hili".

Clarence Lihundi ambae ni mmoja kati ya wanafunzi walio katika mradi huo anasema kuwa unatoa msingi mzuri wa kuisaidia jamii tangia wakiwa chuoni.

"Sisi kama wanafunzi tunakipongeza chuo hiki kwa kutuunganisha na vituo mbalimbali vinavyosaidia waathirika wa dawa za kulevya kwa kuwa tumepata wasaha wa kufanya kazi kwa vitendo zaidi" anasema Clarence.

Khamis Shuwira ambae ni meneja mradi wa kituo cha Chance to change Sober house kilichopo Mbezi anasema kuwa ujio wa wanafunzi hao katika kituo hicho ni sehemu mojawapo ya kuongeza nguvu katika kuwasaidia vijana kuachana na dawa hizo.

Anasema kuwa kwa kuwa wanafunzi hao ni vijana na wamefundishwa masuala mbalimbali katika kukabiliana na dawa hizo hivyo wataongeza nguvu katika ushauri wa kuwaepusha vijana kuendelea na matumizi hayo.

Lakini hata hivyo anaongeza kuwa waathirika wa dawa za kulevya pia wanatakiwa kuunganishwa kwa ukaribu zaidi na wataalamu wa afya, wanasheria pamoja na wahusika wengine.

Anasema kuwa katika vituo vingi hakuna wataalamu wa kutosha wa kutoa huduma za afya kwa waathirika hasa wengi wao hawapatikana katika muda mwafaka wanapokuwa wakitafutwa.

Anafafanua zaidi kuwa kuna wakati waathirika wanakabiliwa na magonjwa mengine kadhaa lakini wakihitaji msaada wa wataalamu wa afya kunakuwa na shida kuwapata.

"Madaktari wengi wanaomba fedha kwanza kila pale ambapo wakiwa wanaomba kuitwa kuja kusaidia vijana na sisi fedha sio kwamba tunazo ila tunavyanzo kidogo tu vya kifedha kuweza kugharamia" anasema kijana huyo.

Anaongeza kuwa "sasa kama ambavyo KIU imeamua kuwatoa wanafunzi wake kuja kusaidia harakati za kuwasaidia vijana basi ni sisi pia tunaona kuwa hata wadau wengine nao wafanye hivyo hivyo".

KIU imeanzisha mradi huo wa Center for Wellness and Social Innovation ambao umepania kuhusisha nguvu ya kitaaluma na kiutalaamu kutoka chuoni hapo katika kuisaidia jamii ya kitanzania.
======================= 

Thursday, October 15, 2015

Shule ya Mtakuja yakumbukwa


PriceWaterhouseCoopers (PWC) donated 563 books, worth TZS 4.1 million to the to the Mtakuja Secondary School (Kinondoni library).  Bachi Shirima of PriceWaterhouseCoopers handed

over books to Lucy Peter, Head of the English Department.  Also present were PWC staff, library prefects and Realising Education/READ International Executive Director, Montse Pejuan.

many thanks,

Saturday, October 10, 2015

Star Time yazungumza na wateja wake, yaahidi makubwa zaidi

Meneja wa Operesheni wa king'amuzi cha Star Time Gaspa Ngowi kulia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana huduma za king'amuzi hicho ikiwa ni sehemu ya huduma kwa wateja wa king'amuzi hicho

Balozi wa kingamuzi cha Star times Shafii Dauda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo king'amuzi hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateaj wa king'amuzi hicho
Habari kamili
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayosherehekewa na taasisi pamoja na makampuni mengineyo duniani kote, kampuni inayotoa huduma za matangazo ya luninga kwa dijitali nchini ya StarTimes imesema kuwa imepiga hatua kubwa katika maboresho ya huduma zake.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa wiki hii hutoa fursa ya kipekee ya kupima huduma wanazozitoa kwa wateja na namna ya kuzifanyia maboresho.

“Tunapokutana na wateja wetu ana kwa ana ndivyo hutuwia urahisi kwetu kuweza kujua wanahitaji nini hasa. Ukizingatia ndani ya wiki hii yote wateja wetu wamehudumiwa na wakuu wa vitengo mbalimbali. Kwa mfano kwa sasa tunafanya jitihada nyingi za kusambaza huduma zetu mikoani ili kuwafikia wateja wengi zaidi wa vijijini.” Alisema Bi. Hanif
Amesema kuwa mpaka hivi sasa Kampuni yake imekwishaifikia mikoa takribani 18 nchini Tanzania na mipango ni kusambaza zaidi kila pembe ya nchi.

“Tunatoa huduma zetu kwa bei nafuu zaidi ili kila mtanzania aweze kumudu lengo ikiwa ni kila mmojawapo afurahie ulimwengu wa dijitali nchini.” Alimalizia
Kwa upande wake Meneja wa Operesheni wa StarTimes Tanzania, Bw. Gaspa Ngowi naye amesema kuwa katika kuboresha huduma zao kampuni imeboresha chaneli za michezo kwa kutambulisha vifurushi vipya mahususi kwa wapenzi wa michezo nchini.

Meneja huyo ametaja kuwa vifurushi hivyo ni vya Sports Play na Sports Plus ambavyo amefafanua kuwa ni kama nyongeza ya vifurushi viwili vilivyopo vya Mambo na Uhuru.

“Hivi sasa wateja wetu wa kifurushi cha Mambo wanaweza kujiongeza kwa kuongeza malipo kidogo ya Sports Play ambapo wataweza kujivinjari na ligi za Bundesliga  ya Ujerumani, Serie A ya Italia na Ligue 1 ya Ufaransa ‘Live’ kupitia chaneli za Sports Arena, Fox Sports na Sports Life.”

Vilevile kwa wateja wa kifurushi cha Uhuru nao wanaweza kuongezea malipo kidogo kwa ajili ya Sports Plus ligi hizo hizo kupitia chaneli za Sports Life, Sports Premium na World Football channels.
Bw. Ngowi aliendelea kwa kusema kuwa machaguo ya vifurushi hivi vipya kunaonyesha kujidhatiti kwa kampuni ya StarTimes katika maboresho, ubunifu na kuwajali zaidi wateja wake hususani wapenzi wa soka kuweza kutazama michuano na ligi mbalimbali kwa bei nafuu.

“Siku zote tutabaki kuwa waaminifu kwa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za kipekee kutoka StarTimes kwa kuwawezesha kufurahia michezo mbalimbali na tena kwa machaguo ya bei zinazolingana na vipato vyao.” Aliongezea
Bei za kifurushi cha Sports Play ni shilingi 5000/- na Sports Plus ni shilingi 14,000/- tu.

“Hii inamaanisha kwamba kwa wateja wa Mambo ambao wanalipa shilingi 12,000/- itabidi waongezee shilingi 5000- ili kupata kifurushi cha Sports Play na wateja wa Uhuru wanaolipia shilingi 24,000/- itabidi waobgezee shilingi 14,000/- ya kifurushi cha Sports Plus,” alisema Bw. Ngowi na Kumalizia, “Kwa kufanya hivyo wataweza kutazama mechi zote Live na pia kwa wateja wa kifurushi cha Kili kuna ongezeko kidogo la bei kwani wao watalipia shilingi 48,000/- na kuweza kupata chaneli zote za vifurushi vya michezo.”

Akitoa maoni juu ya huduma za StarTimes nchini, mtangazaji na mchambuzi nguli wa masuala ya michezo, Bw. Shaffih Dauda amepongeza sana jitihada za kampuni hiyo katika kuunga mkono shughuli za michezo hususani soka.

Amesema kuwa kuonyesha uthubutu wao katika kudhamini ligi ya daraja la kwanza ni tukio linalohitaji pongezo kubwa sana.

“Kwa muda mrefu kilio cha wapenzi na wadau wa soka nchini ni kupata udhamini kwa ligi ya daraja la kwanza ambayo huibui vipaji vingi zaidi tunavyoviona ligi kuu. Kwa udhamini huu wa StarTimes tunaamini kuwa utaongeza hamasa zaidi, utainua ari na pia kufanya ligii hii kuwa yenye ushindani zaidi ambapo soka la Tanzania litajionea timu nzuri zaidi zikitengenezwa na wachezaji wazuri zaidi wakipatikana ambao si hazina tu kwa ligi kuu bali pia hata kwa timu ya taifa na kimataifa.” Alihitimisha Bw. Dauda
Mwisho … ///

Thursday, October 1, 2015

Taasisi ya elimu Tanzania yakopeshwa bilioni 3 na Mamlaka ya Elimu

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Mamlaka ya Elimu (TEA) zilipotialiana saini mkataba wa makubaliano ambapo TEA itaipatia TET Mkopo wa Sh Bilioni 3 kwaajili ya kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita. Prof Mchome, amewataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu inayokidhi viwango vya kimataifa.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Joel Laurent na Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk Leonard Akwilapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakitiliana saini hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakionesha hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET baada ya kutiliana saini jana mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.Picha: Father Kidevu Blog.


Picha ya pamoja ya Wakurugenzi wa TEA, TET, Katibu Mkuu pamoja na watumishi wao.
 **************
Na Father Kidevu Blog
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeipatia mkopo wa shilingi Bilioni 3 Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) katika makubaliano yaliyofikiwa leo Septemba 30, 2015 jijini Dar es Salaam.



Makubaliano hayo yalifikiwa mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Eklimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome ambapo TET itatumia fedha hizo katika kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Joel Laurent amesema mkopo huo nafuu utakaolipwa katika kipindi cha miaka sita, umetolewa katika kutekeleza sera mpya ya elimu ya mwaka 2014.



“Mamlaka kwa kuzingatia Sera mpya ya Elimu ya mwaka 2014, imeridhia maombi ya mkopo ili kuhakikisha uwepo wa mitaala, muhtasari na vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la sita vinavyoendana na mahitaji na wakati,”alisema Laurent.



Utaratibu huo utaiwezesha TET kuandaa vitabu vya kiada kwa hatua ya kwanza ya elimu msingi, kutafanya uwepo wa mitaala inayoendana na kuwa kuboresha mfumo wa upatikanaji wa vitabu sahihi kulingana na mitaala nchi nzima kupitia TET hivyo Sasa nchi itakuwa na kuwa na kitabu kimoja cha kiada kwa shule nzima tofauti na ilivyo sasa kila shule zinavitabu vyake vya kufundishia.



Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk Leonard Akwilapo alisema mkopo huo watautumia kufanya utafiti na kubaini mahitaji ya maboresho kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo wanafunzi, walimu, wazazi na waajiri na kuandaa mitaala ya Elimu ya awali na Elimu ya Msingi kuanzia darasa la tatu hadi sita na kuandika vitabu vya kiada.



Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome aliwataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu inayokidhi viwango vya kimataifa.

Tuesday, September 22, 2015

Wasemavyo wanafunzi wa Marekani kuhusiana na ujio wa Papa nchini humo

Saturday, August 22, 2015

Nini mtazamo wako katika usafirishwaji wa wanafunzi hawa?

Wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko wakiwa wamerundikwa kwenye kiti kimoja cha nyuma ya dereva katika basi litokalo Kariakoo kuelekea Yombo Vituka.

Friday, August 21, 2015

Marufuku kuwafukuza wanafunzi kwa kushindwa kufauku-- Wizara

Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema ni marufuku kukaririsha darasa, kuhamisha au kufukuza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kushindwa kufikisha wastani wa alama za ufaulu wa shule.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Wizara hiyo na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Consolata Mgimba, ilisema Kumejitokeza tatizo la baadhi ya Shule za Sekondari zisizo za Serikali kukaririsha, kuwahamisha au kuwafukuza wanafunzi ambao hawakufikia wastani wa alama za ufaulu uliowekwa na shule. 

Aidha taarifa hiyo ilisema jambo hili ambalo ni kinyume na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi limesababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo na hivyo kupoteza haki yao ya msingi.

“Waraka wa Elimu Namba 12 wa Mwaka 2011 umeeleza wazi kuwa ni marufuku kwa shule kukaririsha darasa, kuhamisha au kufukuza wanafunzi kwa kushindwa kutimiza wastani wa alama za ufaulu uliowekwa na shule,” inasema sehemu ya taafifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema mwanafunzi yeyote aliyedahiliwa kujiunga na masomo anapaswa kuendelea na masomo isipokuwa endapo atashindwa kufaulu mtihani wa kitaifa uliowekwa na Wizara pekee yaani mtihani wa Kidato cha Pili. 

Wizara hiy imetahadharisha shule zote zinapaswa kuzingatia suala hili na hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa usajili wa shule kwa kukiuka taratibu zilizowekwa.

Endapo kuna shule inakiuka taratibu hizi, wazazi au walezi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi au Ofisi za Elimu.
Mwisho

Thursday, July 30, 2015

Fuatiliana kuhusiana na elimu na Tehama

IMG_8896
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
IMG_8887
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
IMG_8817
Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.
Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.
Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.
“Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.
Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
IMG_8793
Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
“Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.
IMG_8775
Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.
Naye kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania na Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi .
Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu na ubora wa walimu.
Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.
Alisema mradi huo utasaidia kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.
Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
IMG_8849
Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.
IMG_8798
IMG_8821
IMG_8787
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.
IMG_8842

habari ya elimu


<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8896.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141475" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8896.jpg" alt="IMG_8896" width="640" height="427" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000080;"><em><strong>Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.</strong></em></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8887.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141476" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8887.jpg" alt="IMG_8887" width="640" height="427" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia  elimu.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco  nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama  na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8817.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141477" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8817.jpg" alt="IMG_8817" width="640" height="427" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000080;"><em><strong>Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha maf</strong></em><em><strong>unzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.</strong></em></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano  ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga  kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong> “Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8793.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141481" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8793.jpg" alt="IMG_8793" width="640" height="427" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000080;"><em><strong> Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.</strong></em></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>“Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu  watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8775.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141482" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8775.jpg" alt="IMG_8775" width="640" height="427" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na  Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Naye  kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa  Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania  na Chuo kikuu cha Dar es salaam.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi .</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu  na ubora wa walimu.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Alisema mradi huo utasaidia  kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000000;"><strong>Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha  hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.</strong></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8849.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141478" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8849.jpg" alt="IMG_8849" width="640" height="426" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000080;"><em><strong>Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.</strong></em></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8798.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141479" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8798.jpg" alt="IMG_8798" width="640" height="426" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8821.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141480" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_8821.jpg" alt="IMG_8821" width="640" height="426" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_87871.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141483" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_87871.jpg" alt="IMG_8787" width="640" height="427" /></a></p>
<p style="text-align: center;"><span style="color: #000080;"><em><strong>Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.</strong></em></span></p>
<p style="text-align: center;"><a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_88421.jpg"><img class="aligncenter size-full wp-image-141484" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_88421.jpg" alt="IMG_8842" width="640" height="427" /></a></p>


KAWAIDA

IMG_8896
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
IMG_8887
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia  elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco  nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama  na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
IMG_8817
Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.
Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano  ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga  kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.
Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.
 “Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.
Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
IMG_8793
 Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
“Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu  watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.
IMG_8775
Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na  Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.
Naye  kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa  Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania  na Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi .
Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu  na ubora wa walimu.
Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.
Alisema mradi huo utasaidia  kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.
Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha  hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
IMG_8849
Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.
IMG_8798
IMG_8821
IMG_8787
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.
IMG_8842