Picha ya Maktaba |
UNAWEZA kudhani ni Hekaya za
Kusadikika! Lakini ni kisa cha kweli kwamba, mama mzazi amemshitaki polisi mwanaye wa kiume ambaye ni
mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16 kwa kile anachodai
amechoshwa na tabia ya mwanaye ya kufanya mapenzi na nguruwe
wao jike mara kwa mara na hata kujikuta akiacha shule.
Amelalamika akidai kuwa kijana
huyo amenogewa `penzi’ la mnyama huyo maarufu hapa kama “kitimoto au Noah”
kiasi cha kumfanya aache masomo na kuwa
mtoro sugu shuleni.
Nguruwe huyo jike
inadaiwa anafugwa na
familia ya mwanafunzi huyo
anayesoma katika shule moja ya umma
ya sekondari, Manispaa ya
Sumbawanga.
Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa
Kitengo cha Polisi Jamii mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa aliyemweleza mwandishi wa habari
hizi jana kuwa, mama mzazi wa
mtoto ameripoti tukio hilo katika jeshi
polisi.
Kibassa amesifu uamuzi huo,
akisema ni mafanikio makubwa yanayotokana na Mpango Shirikishi wa
Kitengo hicho wa kurejesha
shuleni watoto ambao ni
watoro sugu.
Anasema mwanafunzi huyo
(jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule
mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga waliorejeshwa hivi karibuni
kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha
watoro shuleni unaotekelezwa na Kitengo cha Polisi Jamii mkoani humo.
Kwa mujibu wa Kibassa,
wazazi na walezi wenyewe wanafika katika kitengo hicho
cha polisi jamii na kuripoto
kuhusu watoto wao
ambao wamekatiza masomo .
Aliongeza kusema kuwa, wazazi
na walezi hao wanafichua ya
kwamba watoto wao hao licha
ya kutokwenda shuleni, lakini pia nyumbani hawaonekani kwamba baadhi yao
wamebainika kutumia muda wao mwingi kunywa pombe
vilabuni badala ya kusoma.
“Sasa hivi
karibuni ni juzi
tu mama mmoja alinifuata
na kuniripotia kisa cha mwanae wa kiume anayesoma Kidato cha Pili katika shule moja ya sekondari kwamba licha ya kuwa mtoro sugu shuleni; lakini pia
amekuwa na tabia chafu ya kufanya
mapenzi na nguruwe wao
jike mara kwa mara ….
Nilipomhoji kijana huyo alikiri kufanya hivyo …. basi tulimnasihi, “ alieleza.
Kwa mujibu wa Kibassa
baada ya kumsihi mwanafunzi huyo alikubali kuendelea na masomo ambapo
alirejeshwa shuleni kwake na
kupokelewa na walimu na wanafunzi wenzake kwa furaha.
Daktari wa Tiba ya Binadamu, Dk Paulo Maiga akizungumzia tukio hilo alikiri kuwa
mwanadamu kufanya mapenzi na mnyama kuna madhara makubwa ikiwemo kuambukizwa
virusi ambavyo vikingia
mwilini mwa binadamu kuna uwezekano mkubwa visiweze kutibiwa .
“Hili ni tatizo
kubwa madhara yake ni
makubwa huyu nguruwe anaweza kuwa ameshambuliwa na virusi vya ugonjwa ambao ukiingia na kumshambulia mwanafunzi
huyo upo uwezekanao mkubwa
kusiwepo na tiba,“ alisisitiza Dk. Maiga.
0 comments:
Post a Comment