Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, April 21, 2014

Wanafunzi wa vyuo wawataka Ukawa kujea bungeni


Chanzo gazeti la Habarileo

WANAFUNZI kutoka vyuo 10 vya elimu ya juu nchini, wamewasihi wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba kuendelea na majadiliano. 


Waliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana jijini Dar es Salaam na kushutumu hatua yao ya kususia vikao vya Bunge hilo wakisema kitendo cha kueneza propaganda chafu kuhusu Katiba mpya nje ya ukumbi wa Bunge,  hakikubaliki.


Kiongozi wa wanafunzi hao, Gulatone Masiga alisema umoja wa wanafunzi hao haukubaliani na kitendo hicho cha Ukawa cha kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.


Alisema  wanafunzi wanawaomba  wabunge wanaounda umoja huo kuendelea na majadiliano yenye maridhiano ndani ya Bunge hatua itakayowafanya wathibitike kuwa walikuwa na dhamira ya dhati ya kuwapatia Watanzania  Katiba mpya.


 “Katiba mpya haitapatikana kwa Ukawa kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma. Tunawaomba warejee bungeni vinginevyo warejeshe posho walizochukua,'' alisema Masiga ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Wanafunzi hao pia walipinga lugha za kuudhi na kashfa zinazotolewa na baadhi ya wajumbe wa Ukawa  kwa waasisi wa Taifa ambao waliweka msingi mzuri wa Taifa kwa kuwawezesha wananchi wakiwemo viongozi wa umoja huo, kupata elimu, kuwa na uhuru wa kujieleza na kupata huduma nyingine za jamii wanazoendelea kufaidika nazo mpaka sasa.


“Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Marekani, Uingereza na nchi nyingine zilizoendelea zina nguvu kubwa kutokana na umoja na mshikamano wao. 

Kitendo cha baadhi yetu kufanya mchezo na Muungano wetu hakikubaliki hata kidogo,”  alisema.

Kwa upande wake, mwanafunzi Dorcas Mwasunda kutoka Chuo cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) alisema inawezekana Ukawa wakawa na hoja nzuri ya kutetea mfumo wa serikali tatu wanaoutaka lakini si vema kwao kutetea sababu hizo nje ya Bunge Maalumu la Katiba.


Alitaka wajumbe  kukubaliana na kuheshimu pia maoni yanayotolewa na wajumbe walio wengi ndani ya Bunge hilo.


Akizungumzia ni kwanini hawakubaliani na mfumo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu ya Katiba, Massoro Hussein Kivuga kutoka Chuo Kikuu cha St John’s, Tawi la Dar es Salaam alisema muundo huo bila ya kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato utasababisha kuwa na Serikali dhaifu ya Muungano ambayo haitaweza kujiendesha.

Hatma ya Ukawa

Bunge Maalumu la Katiba linaendelea na vikao vyake mjini hapa ambavyo licha ya wajumbe kuendelea kujadili hoja kwenye taarifa za kamati, pia hatma ya wajumbe waliosusa Bunge hilo inatarajiwa kujulikana ndani ya wiki hii.  


Hoja iliyoko mezani inayoendelea kuchangiwa na wajumbe ni kuhusu Kamati ya Bunge hilo namba moja hadi 12, juu ya Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba.


Wakati mjadala huo ukisubiriwa kuendelea, wajumbe wanaounda  Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa ) waliosusa Bunge wiki iliyopita,  wamekaririwa wakisisitiza kutorejea bungeni. 


Hata hivyo wiki iliyopita, Mjumbe wa Bunge hilo Maalumu, Mwigulu Nchemba aliomba mwongozo akitaka Mwenyekiti wa Bunge kumwandikia barua Rais  atengue uteuzi wa  wajumbe waliounga mkono kauli ya mjumbe Profesa Ibrahim Lipumba ya kutoka nje ya Bunge wakati wa mjadala. 


Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu alisema mwongozo huo utatolewa baadaye baada ya Kamati ya Bunge ya Uongozi kukutana kujadili jambo hilo, Alhamisi iliyopita. 


Mwongozo huo haukutolewa baada ya kamati hiyo kukutana kwani  Bunge liliahirishwa mchana siku hiyo kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka jambo ambalo linatarajiwa leo, mwongozo husika kutolewa bungeni. 


Wajumbe wanaounda Ukawa, walitoka bungeni kwa kile walichodai wamechoshwa na ubaguzi na matusi dhidi ya CUF, Chadema na Wapemba ndani ya bunge hilo kunakofanywa na wajumbe wa upande wa walio wengi bungeni.


Mjadala
Ingawa haijulikani hatima ya Bunge hilo bila uwapo wa wajumbe hao wa Ukawa, wajumbe waliobaki  wataendelea kuchangia hoja kwenye taarifa za Kamati ya Bunge hilo. 


Sura ya kwanza ya rasimu hiyo ina sehemu mbili, moja inahusu jina, mipaka, alama, lugha na tunu za Taifa na sehemu ya pili  inahusu mamlaka ya wananchi, utu na uhifadhi wa Katiba. Aidha, Sura ya sita inahusu Muundo wa Jamhuri ya Muungano.

Mgawanyiko


Mgawanyiko ulio ndani ya Bunge Maalumu la Katiba ni baina ya wanaounga mkono hoja ya kuwepo kwa muundo wa serikali mbili na wa serikali tatu. Kwa wanaounga mkono serikali mbili, wanasema ndiyo itakayodumisha na kuimarisha Muungano wa Tanzania na kwamba serikali tatu itavunja Muungano.


Kundi hilo linalounga mkono muundo huo linajiita Tanzania Kwanza na wajumbe wake ni kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), TLP , Chausta, Tadea, CCK, Jahazi Asilia, APPT-Maendeleo, UPDP, Wakulima AFP, UIND, ADC, SAU na baadhi ya wajumbe wa kundi la wajumbe 201 .


Kundi la pili ni lile  linalounga mkono hoja ya serikali tatu ambalo ni wajumbe kutoka vyama vya Chadema, CUF, DP , NCCR-Mageuzi na baadhi ya vyama vingine vya siasa pamoja na baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 walioteuliwa na Rais.

Kundi hilo la Ukawa ambalo hata hivyo limesisitiza halitarejea bungeni, hoja yao ni kuwa muundo wa serikali tatu  ndiyo suluhu ya matatizo na kero za Muungano.


Madai ya Ukawa ni kwamba  wajumbe wa Bunge wanaendekeza ubaguzi, matusi na rasimu inayojadiliwa siyo iliyowasilishwa na Tume. 


Baada ya kususia Bunge hilo, siku iliyofuata, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta aliwataka warudi akisema kama lipo jambo, walipeleke kwenye Kamati ya Maridhiano  lizungumzwe kwani kususia Bunge siyo sahihi. 


Wajumbe hao wamesusia Bunge Maalumu la Katiba siku chache kabla ya kuahirishwa kwake Ijumaa wiki hii kupisha maandalizi ya Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. Bunge la Katiba litarejea tena Agosti mwaka huu.

Kamati ya Uongozi

Ingawa uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba haukupatikana jana kueleza hatma ya Bunge baada ya baadhi ya wajumbe kususa, taarifa zilizopatikana ni kwamba Kamati ya Uongozi imeshauri yatafutwe maridhiano.

Julieth katika graduation yake ya kidato cha sita Tusiime


Kwaya ya wanafunzi  ikatumbuiza

Ofisa elimu kwa mkoa wa Dra es salaam Raymond Mapunda ndio alikuwa mgeni rasmi

Elizabeth akipewa zawadi

Eliza akipewa zawadi ya maua na ndugu yake

Add caption

Akakutana na ndugu yake mwengine nje

Alikuwa mwenye furaha

Akiwa na mama yake na rafiki yake

Akiwa na baba yake

akamvalisha taji

Na mama na baba yake

Picha ya pamoja

Huyu ni mwanafunzi ambae nae alihitimu siku hiyo

Thursday, April 17, 2014

Proin kupitia TMT yazidi kuchanja mbuga kutafuta vipaji vya uigizaji

CODES:

SHINDANO la kusaka vipaji vya uigizaji linaloandaliwa na kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa filamu, Proin Promotion limewanasa washindi watatu kutoka mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Kampuni hiyo Josephat Lukaza aliwataka washindi hao kuwa ni Joyce Rebeca, Moses Obunde na
Mwinshehe Mohamed.


Washindi hao wamepatikana kutokana umahiri wao wa kuigiza walioonesha kwenye shindano hilo maarufu kama Tanzania Movie
Talent.


Alisema kuwa kila mmoa alijinyakulia zawadi ya Shilingi  500,000 ambapo washiriki 500 walijitokeza na watano ndio waliofanikiwa kuingia fainali.


Alisema kuwa baada ya kuingia watano katika fainali hizo walichaguliwa washindi watatu ambapo kulikuwa na mshiriki mmoja, Idrisa Ally (40), alionesha kipaji cha hali ya juu cha kuigiza na kuzawadiwa na majaji laki moja.


Alisema kuwa hata hivyo mshiriki huyo hakuchaguliwa kwa kuwa umri wake ulikuwa juu ya umri uliowekwa ambao ni kuanzia miaka 14 hadi 35.


"Fainali za mashindano haya zinatarajiwa kufanyika Agost mwaka huu na tumebaini mengi katika suala hili la kuigiza wapo wenye uwezo mkubwa lakini ndio hivyo umri wao umeenda sana"alisema Lukaza.

Shindano hilo linasimamiwa na majaji wake ambao Yvonne Chery maarufu kama Monalisa pamoja na Single Mtambalike maarufu kama Richie
Richie.
Mwisho

Friday, April 4, 2014

Jerry Slaa na kiu ya kutatua kero za elimu Ilala

DSC_0428
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akiwasili kwenye shule ya sekondari Pugu kwa ajili ya kukabidhi madawati 300 kwa shule tatu zilizopo manispaa ya Ilala na kulakiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jovinus Mutabuzi.(Picha zote na Zainul Mzige).
.Ni katika Mpango wa “Mayor’s Ball” “Dawati ni Elimu, Kalisha mmoja, boresha Elimu”.
Na Zainul Mzige
“Kiongozi hapaswi kutegemea nguvu za Serikali kufanya shughuli za maendeleo” Hayo ni maneno ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa katika hafla ya kukabidhi madawati kwa shule tatu za sekondari zilizopo Manispaa ya Ilala iliyofanyika Shule ya sekondari Pugu.
Katika hafla hii, jumla ya madawati 300 yenye thamani ya shilingi milioni 45 za kitanzania yaligawiwa kwa shule 3 zilizopo manispaa ya Ilala ambazo ni Shule ya sekondari Pugu (107), Shule ya sekondari Ulongoni (93) na Shule ya sekondari Jangwani (100) kupitia jitihada zake za kuanzisha mpango wa Mayor’s Ball 2013 ulioanza mwaka jana kupitia kampeni ya “Dawati ni Elimu, Kalisha mmoja, boresha Elimu”.
Bwana Silaa alitoa pongezi na shukrani za dhati kwa wote waliotimiza ahadi zao katika kufanikisha zoezi zima la ununuzi wa madawati mapya na kufanikisha kampeni yenye lengo la kuinua viwango vya elimu ya sekondari na msingi Tanzania. Pia, alichukua nafasi kuwaomba wadau waendelea kujitokeza kuchangia elimu kwani ni mara ya kwanza kwa jambo hili la “Mayor’s Ball” kufanyika nchini.
DSC_0431
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akisaini kitabu cha wageni katika shule ya sekondari Pugu mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
“naomba nitumie nafasi kuwapongeza wadau wote walioitikia wito huu na naomba kutoa rai kwa wale wote walioahidi kutimiza ahadi zao ili kufanikisha lengo la kampeni hii iliyobeba kauli mbiu ya Dawati ni Elimu kalisha mmoja, boresha elimu”, alisema Mstahiki meya Jerry Silaa.
Katika hotuba yake, amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii hasa baada ya kuwaboreshea mazingira ya kusomea kwa msaada wa madawati mapya na ya kisasa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Imelda Samjela, ameiomba serikali kuu kuiangalia shule ya Sekondari Pugu kwa jicho la pili kutokana na hadhi yake ya kutoa viongozi nchini na kuifanya iwe na hadhi ya kimataifa. Shule ya sekondari Pugu inajivunia sifa ya kuwa shule iliyozaa viongozi shupavuTanzania akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bi. Imelda aliongeza kuwa kila mwaka tunapoadhimisha Maisha ya Mwalimu Nyerere basi kufanyike jambo aidha kupaka rangi na kusafisha mazingira ya shule hiyo iliyobeba historia ya Taifa la Tanzania. Diwani pia alitoa wito wa kuweka fungu la fedha za kukarabati majengo ya shule hiyo pamoja na kutokomeza kero ya Kunguni shuleni.
DSC_0446
Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi(mwenye suti nyeusi) akizungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa. wengine pichani ni wakuu wa shule za sekondari Ulongoni na Jangwani waliojuika katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati.
Kunguni wamekuwa ni kero kubwa kwa wanafunzi hasa wakati wakulala. Alitoa angalizo hili kwa mwenyekiti wa huduma za jamii.
Akitoa ufafanuzi wa suala la ukarabati wa majengo ya shule hiyo, Mwenyekiti wa huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, Bi. Angelina Nalembeka amesema kuwa Manispaa ilishatoa shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ukarabati na wanampango endelevu wa kufanya hivyo kila mwaka. Mpango huu si tu kwa shule ya Pugu bali kwa shule nyingine pia zinazoizunguka manispaa ya Ilala.
Mwenyekiti huyo pia alithibitisha kufanyika kwa zoezi la awali la kutokomeza Kunguni shuleni kwa kunyunyiza dawa na kuwepo kwa mpango endelevu wa kunyunyiza dawa ili kuondoa kabisa kero hiyo ya Kunguni shuleni.
DSC_0456
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipitia moja ya mafaili ya taarifa za shule hiyo.
“Mheshimiwa Diwani amefuatilia suala lenu la Pugu kwa umakini na taarifa zake tunazo katika Halmashauri. Mwalimu mkuu atakuwa shahidi na tumeshakuja kupiga dawa na bado mwaka huu tutakuja kupiga dawa tena kuondoa Kunguni” alisema Mwenyekiti, Huduma za Jamii.
Aidha, Mwenyekiti wa huduma za Jamii Manispaa ya Ilala aliongeza kuwa suala ya kero la Maji liko kwenye utatuzi kamati yake ya manispaa yake ilishatembelea shuleni hapo na kuona kero hiyo.
Amempongeza Mstahiki Meya kwa juhudi zake za kutatua tatizo la madawati na ameomba wengine pia ambao ni viongozi wakubwa serikalini waliosoma shuleni hapo wakumbuke walipotoka na kusaidia kuiweka katika hali nzuri.
DSC_0479
Meza kuu ikipokea heshima ya ukaribisho kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Pugu (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Kaimu Diwani wa Upanga Magharibi, Bi. Jokha Lemki, Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, Mstahiki Meya, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabazi na Mwenyekiti wa Hudama za Jamii Manispaa ya Ilala, Angelina Malembeka.
DSC_0490
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi akielezea furaha yake ya kupokea madawati 107 yaliyotolewa na mpango wa Mayor's Ball 2013 kupitia kampeni ya "Dawati ni Elimu" chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
DSC_0521
Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, akiwasilisha kero ya shule ya Sekondari Pugu kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhusiana na wadudu aina ya Kunguni kwenye mabweni ya wanafunzi shuleni hapo ambapo imekuwa kero kubwa wakati wa kulala na kuwasababisha usumbufu.
DSC_0524
Sehemu ya madawati kati ya 300 yaliyotolewa na mpango wa Mayor's Ball 2013 kupitia kampeni yake ya "Dawati ni Elimu" inayolenga kutatua uhaba wa madawati kwa shule zilizomo ndani ya Manispaa ya Ilala.
DSC_0546
Mwenyekiti wa huduma za jamii manispaa ya Ilala, Angelina Nyalembeka akitoa ufafanuzi kuhusiana na kero za wadudu aina ya Kunguni katika shule hiyo ambapo amesema mwaka jana walipulizia dawa kwenye mabweni yote ya wanafunzi na haraka iwezekanavyo ataliwasilisha kero hiyo kwenye vikao vya Manispaa na kupatiwa ufumbuzi na wanafunzi waweza kukaa kwa amani bila usumbufu.
DSC_0572
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa, akizungumza na waalimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu, kabla ya kukabidhi madawati kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
DSC_0527
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu wakifuatilia risala ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.
DSC_0622
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha tatu ambaye ni mlemavu Voster Peter wakati akikabidhi madawati shuleni hapo.
DSC_0482
Baadhi ya viongozi wa Kata ya Pugu, Gongo la Mboto na Upanga Magharibi waliohdhuria hafla hiyo.
DSC_0626
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahi jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi, wakati hafla fupi ya kukabidhi madawati 107 kwa shule hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa huduma za jamii manispaa ya Ilala, Angelina Nyalembeka akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela.
DSC_0631
Sasa mtajinafasi wakati wa masomo darasani si ndio..? Mstahiki Meya Jerry Silaa akimuuliza mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Pugu alipokuwa akikabidhi madawati.
DSC_0638
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ulongoni, Bi. Sikitiko Salehe,( wa pili kulia) akipokea moja ya madawati kati ya 93 kwa niaba ya shule yake kutoka kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa ikiwa ni zao la matunda ya Mayor's Ball 2013 iliyoweka kipaumbele kwenye elimu kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule ya sekondari Pugu jijini Dar.
DSC_0645
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Pugu wakionyesha nyuso za furaha isiyo na kifani walipokabidhiwa madawati 107 na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
DSC_0661
Mstahiki Meya Jerry Silaa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali Kata za Gongo la Mboto na Pugu.
DSC_0669
DSC_0674
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa shule ya sekondari Pugu mara baada ya kukabidhi madawati 107 kwa shule hiyo.
DSC_0678
Kaka mkuu wa shule ya Sekondari Pugu, Nicetas Ndekubali Ndeng'asso, akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
DSC_0692
Kaka mkuu wa shule ya Sekondari Pugu, Nicetas Ndekubali Ndeng'asso akipeana mkono na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
DSC_0701
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiondoka shuleni hapa mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi madawati kwa shule hizo za sekondari za manispaa ya Ilala.