Na Evance Ng'ingo
SHIRIKA lisilo la Kiserikali lijishughulishalo na mafunzo na maendelezo ya Muziki la Music Mayday litaendesha shindalo lake la nne la kutafuta vipaji litakalofanyika Machi Mosi mwaka huu.
Shindano hilo litafanyika katika kwenye ukumbi wa ndani ya New Msasani Club uliopo katika kituo cha daladala cha Drive In karibia na Ubalozi wa Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Afisa Mtawala wa shirika hilo Ana Nyerere ilisema kuwa vijana zaidi 15 wanatakiwa.
Alisema kuwa tukio hilo litakuwa ni la kumalizia mfululizo wa mashindano ya kutafuta vipaji yaliyofanywa na Music Mayday kwenye mradi wa “Sounds of Tomorrow” (Sauti za kesho) sehemu nyingine mbalimbali.
"Vijana 15 wa ziada wenye vipaji watachaguliwa kupewa udhamini wa miaka miwili kujifunza chombo au sauti, mafunzo ya kitaaluma katika sauti na ujuzi wa ala au chombo ukarabati na matengenezo"alisema Ana.
"Hivyo basi naomba tena sana sana wasichana jamani mjitokeze kushiriki na kuonyesha vipaji vyenu siku hiyo ili muweze na nyie kuchaguliwa"alisema Ana.
Alisema kuwa washindi hao watajiunga na wenzao waliochaguliwa tayari katika eneo la Max Bar, Ilala ili kuanza mafunzo ya kitaalamu ya muziki kwa miaka miwili Aprili 2014 katika kituo cha mafunzo ya muziki kilichopo Mikocheni A.
Alisema kuwa katika shindano la muziki washindi 15 kati ya washiriki wote watachaguliwa na jopo la majaji ili kupewa udhamini wa muda wa miaka miwili kwa ajili ya elimu ya kitaaluma katika muziki na usimamizi.
Alisema kuwa watapata mafunzo ya kitaaluma katika sauti na ujuzi wa ala, chombo ukarabati na matengenezo , nadharia ya muziki, usimamizi wa muziki, kudhamini na masoko binafsi, uzalishaji muziki kiufundi na usimamizi wa sauti.
Aliongeza kuwa "washiriki wote na watu walioguswa wanaalikwa kutembelea Kituo cha mafunzo ya muziki kilichopo Mikocheni A karibu na shule ya Feza, Mikocheni A kwa kufahamu zaidi utendaji wet wa kazi".
Mwisho
0 comments:
Post a Comment