Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, August 22, 2015

Nini mtazamo wako katika usafirishwaji wa wanafunzi hawa?

Wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko wakiwa wamerundikwa kwenye kiti kimoja cha nyuma ya dereva katika basi litokalo Kariakoo kuelekea Yombo Vituka.

Friday, August 21, 2015

Marufuku kuwafukuza wanafunzi kwa kushindwa kufauku-- Wizara

Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema ni marufuku kukaririsha darasa, kuhamisha au kufukuza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kushindwa kufikisha wastani wa alama za ufaulu wa shule.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Wizara hiyo na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Consolata Mgimba, ilisema Kumejitokeza tatizo la baadhi ya Shule za Sekondari zisizo za Serikali kukaririsha, kuwahamisha au kuwafukuza wanafunzi ambao hawakufikia wastani wa alama za ufaulu uliowekwa na shule. 

Aidha taarifa hiyo ilisema jambo hili ambalo ni kinyume na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi limesababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo na hivyo kupoteza haki yao ya msingi.

“Waraka wa Elimu Namba 12 wa Mwaka 2011 umeeleza wazi kuwa ni marufuku kwa shule kukaririsha darasa, kuhamisha au kufukuza wanafunzi kwa kushindwa kutimiza wastani wa alama za ufaulu uliowekwa na shule,” inasema sehemu ya taafifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema mwanafunzi yeyote aliyedahiliwa kujiunga na masomo anapaswa kuendelea na masomo isipokuwa endapo atashindwa kufaulu mtihani wa kitaifa uliowekwa na Wizara pekee yaani mtihani wa Kidato cha Pili. 

Wizara hiy imetahadharisha shule zote zinapaswa kuzingatia suala hili na hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa usajili wa shule kwa kukiuka taratibu zilizowekwa.

Endapo kuna shule inakiuka taratibu hizi, wazazi au walezi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi au Ofisi za Elimu.
Mwisho