
SEKTA ya Elimu imefanikiwa kwa asilimia 81 na kushika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).Matokeo ya utekelezaji wa mikakati iliyowekwa na BRN ni kupanda kwa ufaulu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la Saba) na kupanda ufaulu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne).Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliyasema hayo bungeni jana...