Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Black Fox Model, Aj Mynah akizungumza na vijana
waliojitokeza kujifunza fani ya uanamitindo katika klabu ya Paparazi iliyopo
Sleep way Masaki.
|
Somo likiendelea na Aj kwa sasa anawafundisha kuhusiana na fursa zilizopo kwenye fani hiyo kuanzia maslahi na mengineo |
Wanafunzo wa uanamitindo wakiwa wamepozi wakionesha njonjo zao baada ya kunolewa na AJ |
Wanafunzo
wa uanamitindo wakiwa wamepozi wakionesha njonjo zao baada ya kunolewa na AJ
|
I really like her initiatives, she so amazing |
AJ akiwa
amepozi na wanamitindo hao wanafunzi katika klabu hiyo ambapo hukutana kila
Jumapili kuanzia saa tatu asubuhi kujifunza mambo yote yahusuyo uanamitindo
|
Na Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO AJ Mynah ameanzisha mpango wa kutoa mafunzo ya
bure kwa vijana mbalimbali wenye vigezo vya kuwa wanamitindo katika klabu ya
Paparazi iliyopo Sleep Way Masaki.
Aj anatoa mafunzo hayo kupitia kampuni yake ya Black
Fox Model ambapo akizungumzia kuhusiana
na sababu zilizopelekea kuanzisha mafunzo hayo alisema kuwa kampuni yake hiyo
imeamua kutoa mafunzo hayo bure kwa vijana baada ya kutoridhishwa na maendeleo
ya fani hiyo hapa nchini.
Mwanadada huyo ambae aliwakuwa mwanamitindo wa Tanzania nje
ya nchini akifanya kazi zaidi nchi za Ulaya alisema kuwa wapo vijana wengi wana
sifa nzuri za kuwa wanamitindo lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na
kutokuwa na uelewa wa kutosha wa fani hiyo na pia hawajahamasishwa.
Aliongeza kuwa anaona kuwa vijana wa kitanzania
wakijihusisha na fani hiyo wanaweza kufika mbali pia hata kufikia hatua ya
kuiwakilisha Tanzania kimataifa zaidi.
Alisema kuwa "Unaweza kuwaona wadada au wakaka ambao
wanavutia kuwa wanamitindo na ukiwauliza kama wamewahi kufikiria kujihusisha na
fani hiyo utakuta labda hata wazo hawana na wengine hawaoni fursa za zitokanazo
na fani hiyo"
Aliongeza kuwa " Kwa sasa nimeamua kuanzisha kampuni
hii kwa lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanaandaliwa vema na kuja kuwa
wanamitindo wakubwa ambao wanaweza kutangaza bidhaa mbalimbali za ndani na nje
ya nchi na kila Jumapili tunakuwapo hapa klabu ya Paparazi, Sleep Way Masaki na
ni bure kabisa kwa vijana kuja kujifunza".
Aliongeza kwa sasa kampuni hiyo ina wanamitindo 40 wakiwamo
wa ndani na nje ya Mkoa wa Dar es salaam.
Akizungumzia kuhusiana na fursa zilizopo kwenye fani hiyo
alisema kuwa yapo makampuni mengi ambayo yanaweza kuwalipa vijana mamilioni ya
fedha ili kutangaza bidhaa zao na vijana wanamitindo ndio pekee wenye kuweza
kufanya kazi hiyo.
====================