Walimu wawili wa shule ya Msingi Nzogimlole wilayani Nzega Mkoani Tabora wamejikuta katika wakati
mgumu baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya na mzazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Selemani Juma baada ya walimu hao kumurudisha shule mwanafunzi Shaabani Mziku kutokana na kuchanika kwa sare yake ya shule (bukta).
Mwandishi wa habari hii alifika katika shule hiyo ya Msingi Nzogimlole na kuzungumza na mwlimu mkuu msaidizi Emmanuel Josephat alisema kuwa mwanafunzi huyo Shaaban Maziku aneyesoma Darasa la pili aliambiwa na mwalimu Richard Zakari aliyekuwa akifundisha katika Darasa hilo kum rudisha nyumbani kutokana na sare yake Bukta kuchani hadi kupelekea sehem zake za siri kuonekana.
Akizungumza kwa simanzi na majonzi mwalimu huyo mkuu msaidizi alisema kuwa motto huyo alifika
nyumbani na kumueleza Baba yake Selemani Juma kuwa mwalimu Rchard alichana bukta hiyo na kumwambia akamwambie Baba yake aishone.
Alisema kitendo hicho kilimfanya mzazi huyo kufika shuleni na kuanza kutoa lugha chafu shuleni hapo
dhidi ya mwalimu na hatimaye kuanza kutoa kipigo kwa waalimu hao hali iliyopelekea wananafunzi waliokuwa madarasani kutoka na kuanza kulia kutokana na kipigo hicho ambacho walikuwa wakipigwa waalimu hao.
Akitumia mawe kurushakwa walimu hao na baadae kutumia fimbo ambayo ilifahamika kwa jina fito
iliyotumika kuwa chapa waalimu hao sehemu mbalimbali katika miili yao hadi
kusababisha majeraha.
‘’Mwalimu hana kosa kwani mtoto kaptura yake ilikuwa imechanika vibaya sana hali iliyopelekea sehem zake za siri kuonekana sasa hatupaswi tuwaache hivi watoto alimwambia akamwambie baba yake aishone ile sare lakini mambo hayakuwa hivyo’’alisema mwalimu.
Akizungumza baada ya kutoka katika Hospitali ya kijiji hicho mwalimu Richard Zkaria alisema kuwa
hali yake inaendelea vizuri na kuongeza kuwa sababu ya kupigwa na mzazi huyo haijui kutokana na jukumu alilolifanya ni la kawaida
Alisema kuwa alipigwa yeye na mwalimu mwenzake Elias Kafiku ambaye alikuwa akiamua ugomvi huo kwa mazazi huyo na kumtaka aingie ofisni ili suala hilo waweze kulizungumza kiofisi na kufikia muafaka hata hivyo mwalimu huyo alipigwa.
Mtendaji wa kijiji hicho ………alisema kuwa tukio hilo limetokea July 25 mwaka huu katika shule hiyo
ambapo waalimu wa wili walipigwa na mzazi kisha kujeruhiwa vibaya na mzazi
huyo.
Alisema kuwa jitihadi mbalimbali zakumkamata mzazi huyo zilifanyika baada ya migambo wa kijiji jirani
kumkata kisha kupelekwa katika kituo kidogo cha polis cha bukene ili hatua
mbalimbali za kisheria ziweze kushika mkondo wake.
‘’Nawaomba wazazi na walezi wabadilike wajari elimu pia matukio kama haya wafuate taratibu sahihi za
kiofisi kwani kujichukulia maamuzi kuna madhara yake’’alisema mtendaji
Wakizungumza kwa muda tofauti wananchi wa kijiji hicho cha Nzogimlole walisema kuwa kitendo hicho
kilichofanywa na mzazi huyo sikizuri kutokana na kujichukulia sheria mkononi
hali ambayo ilipelekea uzalilishaji mbele ya waalimu pamoja na kuwapatia hofu
waalimu wengine wa shule hiyo.
Mwalimu Elizabert Kafurila alisema tukio hilo limewatia hofu katika utendaji kazi kutokana na
wazazi kuingilia majukumu ya waalimu na kuongeza kuwa wazazi wanapaswa
kujirekebisha na nkufuata taratibu maalumu za Ofisi.
Kamanda wa polisi mkoani wa tabora Suzani Kaganda alisema kwamba mzazi huyo nashikiliwa kwa tuhuma za kupinga na kujeruhi vibaya na hatarifikishwa mahakamani baada ya upepelezi
kukamilika.
Mwisho.