WAZIRI wa Wizara ya Habari,Utamadun, Vijana na Michezo Fennela Mukangara jana alikabidhi vifaa vya michezo kwa shule za sekondari 12 zitakazoshiriki ligi ya Dar es salaam Community Sports Cup.
Ligi hiyo maalum kwa ajili ya kuandaa wanamichezo bora wa baadae itaanza Februali 8 mwaka huu na kushirikisha sekondari zilizopo wilaya ya Ilala, Kinondoni na Temeke chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom n aimehasisiwa na waziri huyo.
Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo, Mukangara alisema kuwa michezo ni biashara kamii ambayo inapaswa kuwekezwa kwa ajili ya manufaa ya baadae.
Alisema kuwa ili kuwa na ligi bora ya baadae ni vema maandalizi yakaanzia kwa sasa tena katika kuwandaa wanafunzi tangia wakiwa shuleni.
Alisema kuwa kilichomsukuma kuhasisi Ligi hiyo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na wanamichezo imara wa baadae wenye kuwa na misingi mizuri ya michezo.
Alisema kuwa kwa sasa mradi huo uliopo kwenye majaribio umeanza na mchezo wa soka lakini kwa baadae itahamia katika michezo mingine kama vile Netiboli na mingineo.
Pia aliwataka Maofisa Tawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanakuwa na maandalizi mapema ya kuziandaa sekondari kushiriki ligi kama hiyo ambayo baadae itafika hadi mikoani.
"Nawaagiza Maofisa Tawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanajipanga ili pindi ligi hii itakapofika mikoani mwao waweze kuiendesha pia"alisema Mukangara.
Meneja Mawasiliano wa nje wa Vodacom, Salum Mwalimu alisema kuwa kampuni hiyo imeridhishwa na michezo hiyo na kuamua kudhamini vifaa vya michezo.
Vodacom ilitoa mipiri, viatu, kombe na vifaa vingine muhimu vya michezo kwa wanafunzi hao.
Kwa upande wake msimamizi wa Ligi hiyo kutoka Sekondari ya Kibasila, Abel Mtweve alisema kuwa katika shule 12 zinazoshiriki ligi zitakuwa zikicheza kila siku ya Jumamosi na Jumapili katika wilaya zao.
Alisema kuwa katika mechi mbilimbili zitakazokuwa zikichezwa na timu hizo washindi kutoka kila wilaya watakutana katika ngazi ya nusu robo fainali, nusu fainali na kisha fainali.
Alisema kuwa kwa wilaya ya Temeke kituo kitakuwa katika sekondari ya Kibasila, huku wilaya ya Ilala itakuwa ni Sekondari ya Benjamini Mkapa na kisha Kinondoni itakuwa ni Sekondari ya Tuliani.
Mwisho