Tuesday, October 30, 2012
Friday, October 26, 2012
Benki ya NMB yaendelea na kampeni yake ya kuwambuka wanafunzi, yamwaga madawati
Hasan Majaar Trust Fund (HMTF) yawanusuru wanafunzi kuendelea kukaa chini mkoani Njombe
3:50 AM
No comments
Wanafunzi wakifurahuia baada ya makabidhiano hayo |
"Ngoja tuyajaribu kwanza haya madawati"
Sunday, October 21, 2012
Jionee mwenyewe tofauti ya mazingira ya elimu hapa nchini
12:56 AM
No comments
Hapa wanafunzi wakijadiliana na walimu wao ni katika mazingira ya vijijini hapa
Hapa ni katika shule ya msingi ya Itete iliyopo wilaya ya Nkasi katika mkoa wa Katavi wakiwa wanasoma wakiwa wamekaa chini kabisa darasani. Shule hiyop ilianzishwa mwaka 1988 na inakabiliwa na ukata mkubwa wa madawati huku walimu wakiwalaumu wazazi kwa kushindwa kuchangia elimu kwa shule hiyo na kuchangia kununu madawati.
Hapa wanafunzi wa mjini wakipewa ujumbe na mgeni aliyewatembelea ambapo aliwasihi masuala mbalimbali yahusuyo elimu hapa nchini
Hawa nao ni wanafunzi wa mjini wakijisomea kwa njia ya mtandao. Sasa unaona utofauti wa elimu kulingana na mazingira lakini hawa ambao wamesomea vijijini katika shida utashangaa kuwa hawatapewa hata mikopo

Saturday, October 20, 2012
Friday, October 19, 2012
NMB imefanikisha kwa kiasi kikubwa elimu kwa Mama Shujaa wa Chakula na shindano la Maisha Plus kwa ujumla
7:25 AM
No comments
Baadhi ya watu waliohudhuria siku hiyo
Meneja Masoko wa NMB Imani Kajula akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba
Baadhi ya akina mama walioshiriki shindanoa hilo wakiwa wanasubira mshindi kutangazwa
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba akimkabidhi tuzo mshindi wa shindanoa la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Marta
Habari Kamili
Benki ya NMB imefanikisha upatikanaji wa elimu kwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula lililokuwa liliendelea katiak shindano la Maisha Plus
Elimu iliyotolewa ni pamoja na elimu ya biiashara, kilimo, ujasiriamali na nyinginezo ambapo Meneja Masoko wa NMB, Kajula alisisitiza kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo mingi sana kwa akina mama pia ili kuwawezesha zaidi kimaisha.

UTAMADUNI wa kupika, kula, kulima na kumwagilia vijijini huku wakikutanishwa watu wa makabila, dini na mila tofauti ni utamaduni ambao ni mara chache kuukuta katika jamii zetu.
Ikiwa ni kwa mara ya kwanza kutokea katika shindano la Maisha Plus, ambapo kulikuwa na shindano ndani yake lililojulikana kama Mama Shujaa wa Chakula ndani ya shindano hilo la Maisha Plus.
Katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula akina mama kutoka vijiji, wilaya na mikoa mbalimbali nchini, walipata fursa ya kukaa, kulima, kumwagilia mazao na kula pamoja vyakula vya aina mbalimbali.
Utamaduni kama huu ni mzuri kwa wanajamii ya Tanzania, kwa kuwa ilikuwa ni sehemu mojawapo ya kujifunza masuala mbalimbali ya kijamii, hususan suala la kilimo.
Shindano hilo lililofikia tamati Jumanne iliyopita, lilikuwa ni la kuvutia kwa kuwa akina mama hao kwa siku 14 walizokaa kijijini humo, walipata nafasi ya kupewa elimu ya kilimo, ujasiriamali, haki za kumiliki ardhi, masuala ya afya na pia hata masuala ya katiba pia.
Akizungumza na gazeti hili, Mratibu wa Shindano hilo, Masoud Ali Kipanya, anasema kuwa ameamua kuwashirikisha akina mama wanaojishughulisha na kilimo katika shindano la Maisha Plus 2012 kwa kuwa anatambua mchango wa kilimo katika maendeleo ya nchi.
Kipanya anasema kuwa ili kuongeza motisha ya kutambua, kupenda na kuendeleza kilimo kwa wananchi, ameona kuwa kupitia kipindi hicho ni muda muafaka wao kujionea na kujipatia elimu ya kilimo.
Anasema kuwa wakiwa kijiji hapo, wanawake wamelima, kupanda na kuotesha miche mbalimbali kwa msaada wa kitaalamu kutoka shirika la Oxfam.
“Najua tulizunguka mikoa na wilaya karibia zote hapa nchini kusaka hawa akina mama ambao wamekuja kushiriki katika shindano hili, tunashukuru msaada kutoka kwa shirika la Oxfam kwa kuwa wameonesha nia ya kweli ya kutusaidia katika kufanikisha hatua hii muhimu,” anasema Kipanya.
Jumanne iliyopita ambapo ilikuwa ndio Siku ya Chakula Duniani, washindi walitajwa na kupatiwa zawadi zao.
Mkulima Marta Waziri kutoka wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, ndiye aliyeshinda Tuzo ya kuwa Mama Shujaa wa Chakula mwaka huu.
Mwanamama huyo alipewa zawadi ya vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh milioni kumi, ambapo aliwashinda wenzake 14.
Aliyeshika nafasi ya pili ni Elimiana Eligaesha kutoka wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na wa tatu ni Tatu Abdi. Wote watatu watapatiwa mafunzo ya kilimo na ujasiriamali.
Utamaduni huo unaongeza hamasa kwa vijana na watu wengine waliofuatilia shindano hilo, kwa kuwa mchezo huo wa runinga, ulikuwa unaburudisha na kuelimisha pia.
Kuna changamoto nyingi zinazowakabili wakulima vijijini hasa akina mama. Akinamama hao hawakusita kufikisha ujumbe wao kwa Rais Jakaya Kikwete, wakilalamikia matatizo yanayowakabili.
Katika barua yao ya wazi kwa Rais Kikwete, walilalamikia suala la wawekezaji kupewa kibali cha kumiliki ardhi kwa miaka 99, ambapo walitaka miaka hiyo ipunguzwe hadi iwe miaka mitano.
Pia, walilalamikia kudharauliwa na mabwana shamba kwa kushindwa kwao kutekeleza majukumu yao. Pia, walitoa changamoto kwa waandishi wa habari na wadau wengine muhimu wa serikali, kuhakikisha kuwa wanawasaidia wakulima kiujumla.
Naibu Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alikuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo huo. Anasema ili kumwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika kilimo, anatakiwa kupewa moyo.
Anasema taasisi mbalimbali za kutoa mikopo ya pembejeo za kilimo, asilimia moja ya akina mama ndio hunufaika na mikopo hiyo huku asilimia 99 ya wasiozalisha chakula ndio wanamiliki ardhi.
Anasema hata katika kilimo cha umwagiliaji, wanaume ndio hunufaika zaidi, ikilinganishwa na akinamama hao pia hupata shida katika kupatiwa huduma za ugani.
“Ni kwamba hawa wa akinamama wakulima wana majukumu makubwa na muhimu katika kuzalisha chakula hasa katika ngazi za vijijini, lakini utakuta akizalisha chakula na kuuza, lakini utakuta mume ndio huchukua faida yote na kuondoka nayo,” alisema Makamba.
Meneja Masoko wa Benki ya NMB ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Imani Kajula, alisema kuwa benki hiyo mpaka sasa imeshatumia zaidi ya Sh bilioni 100 kusaidia kilimo.
Anasema kuwa wameweza kutoa elimu ya kilimo na ujasiriamali kwa akinamama, waliokuwepo katika shindano hilo na kwa wanawake wakulima.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Monica Gorman, anasema kuwa shirika lake linatambua namna ambavyo wakulima wanawake wanavyohangaika katika kujiendeleza.
Anasema kuwa wanatakiwa kupewa elimu ya kutosha, kusaidiwa kifedha kwa ku
pewa mikopo pamoja kutokatishwa tamaa.
Shirika lisilo la kiserikali la Kaluwa Development Trust Fund, linahamasishwa na kuwasaidia wakulima wadogo, ambapo liliwakabidhi vifaa vya kilimo akinamama hao.
Shanila Habib Kaluwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo.
Anasema kuwa wakiwa kama wadau wa kilimo mkoani Morogoro na Dar es Salaam, wameshiriki katika kuwasaidia kielimu na kitaalamu akinamama shujaa hao na wengine wa mikoani.
“Najua huu kwanza wa kuwaweka akinamama hapa kijijini na kuwaendeleza kitaaluma katika kilimo ni kitu muhimu, hivyo sisi kama wadau tunatoa pampu za maji na bidhaa nyingine za kilimo na ni vema pia watu wengine wakajitokeza kusaidia suala hilo,” anasema Shanila.
Mwisho
Thursday, October 18, 2012
Fountain Gate Academy shule ya kisasa inafundisha vizuri, wahi sasa
5:45 AM
No comments
Madarasa mazuri na ya kuvutia yanayomwezesha mwanafunzi kusoma kwa amani na utulivu
Kwa kawaida namba na herufi huwa zinavutia katika kupendezesha madarasa kama ambavyo darasa hili likiwa limepambwa na nambari na hivyo kumfanya mwanafunzi kuwa katika hamasa ya kusoma muda wote
Monday, October 15, 2012
Wafanyakazi wa Zantel wapewa elimu ya afya
10:16 AM
No comments
Ili kuweza kuimarisha afya yako ikiwa pamoja na kufahamu namna ya kujirinda na magonjwa mbalimbali inatakiwa kupewa elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya afya pamoja na lishe, pichani wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wakipewa elimu ya afya kiujumla.
Pia kulikuwa na ushauri wa hapo kwa hapo kutoka kwa wataalamu wa masual ya afya
Wafanyakazi wakijadiliana masuala muhimu ya afya wakati wakisubiria kwenda kupima afya zao
PRO wa Zantel Jaquline Matowo akipimwa presha na wataalamu hao
Pia wakapata picha ya pamoja na wafanyakazi wote

Friday, October 12, 2012
Maktaba iliyopo kijiji cha Lushongo wilaya ya Pangani
8:58 AM
No comments
Pembeni yangu ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la Nipashe Lulu George anawakilisha mkoa wa Tanga nilikuwa nae katika ziara hiyo ni pia mwanaharakati wa masuala mbalimbali likiwamo suala la elimu pia
Katika kijiji cha Ushongo kilichopo Pangani vijijini kuna huyu jamaa ameanzisha maktaba yake kijijini humo ambapo anasomesha wanafunzi bure
Sehemu ya mbele ya Maktaba hiyo ambapo ni ndogo lakini kwa vijijini kuwa na Maktaba kama hiyo ni kitu kizuri na cha kuvutia zaidi habari zaidi zinakuja
Katika kijiji cha Ushongo kilichopo Pangani vijijini kuna huyu jamaa ameanzisha maktaba yake kijijini humo ambapo anasomesha wanafunzi bure
Nilipata nafasi ya kuzungumza na mmiliki wa maktaba hiyo
Sehemu ya mbele ya Maktaba hiyo ambapo ni ndogo lakini kwa vijijini kuwa na Maktaba kama hiyo ni kitu kizuri na cha kuvutia zaidi habari zaidi zinakuja
Friday, October 5, 2012
7:40 AM
No comments
Haya dada tuvushe twende shule
7:35 AM
No comments
Watoto hawa wanakisubiria kuvushwa kwenda shule asubuhi katiak eneo la Kigogo ambapo kunakuwa na ajali nyingi za watotoo wadogo
Add caption |